RAIS wa mstaafu wa Marekani, Barack Obama ameeleza namna alivyoguswa na kifo cha Mfalme wa Soka duniani, Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele ambaye amefariki dunia leo tarehe 29 Disemba, 2022. Inaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Obama amesema Pele aliyefariki akiwa na umri wa miaka 82 kwamba alikuwa mchezaji aliyeleqa nguvu ya michezo katika kuunganisha watu.
“Pele alikuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kucheza mchezo huo mzuri. Akiwa kama mmoja wa wanamichezo wanaotambulika na kuheshimika zaidi ulimwenguni, alielewa nguvu ya michezo katika kuleta watu pamoja. Maombi yetu yako pamoja na familia yake na kila mtu ambaye alimpenda mpendwa wetu,” ameandika Obama.
Kifo cha mwanasoka huyo pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu akiwa mchezaji, kilithibitishwa na binti yake Kely Nascimento kwenye mtandao wa Instagram.
Mchezaji huyo wa hali ya juu alikuwa akitibiwa saratani ya utumbo mpana tangu 2021. Alikuwa amelazwa hospitali mwezi uliopita akiwa na maradhi mengi.
Leave a comment