October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Barabara ya Kibena-Lupembe-Madenge-Morogoro kujengwa kwa kiwango cha lami

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa

Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, amesema kutokana na umuhimu wa barabara ya kuanzia Kibena-Lupembe-Madege mpaka Morogoro, Serikali imetenga kiasi cha Sh 8.5 bilioni kuanza taratibu za ujenzi kwa kiwango cha lami. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).

Mbarawa ameyasema hayo leo Alhamisi terehe 11, Agosti, 2022 wakati akihutubia wananchi wa Mtwango mkoani Njombe kwenye msafara wa Rais Samia kuelekea mkoani Iringa.

Amesema umuhimu wa barabara hiyo unatokana na kupita katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa na pia inaunganisha mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Njombe na Morogoro.

Aidha Waziri Mbarawa ameiomba halmashauri ichangie nusu ya gharama za taa za barabarani na kwamba Wizara itachangia nusu.

Kuhusu kupandisha hadhi barabara amesema suala hilo watalifanyia kazi na wakiona kama imekidhi vigezo itapandishwa hadhi na kuwa ya TANROADS.

error: Content is protected !!