July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bara, Z’bar kumaliza utata bei ya umeme

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania na ile ya Zanzibar zitakutana, kujadili na kushughulikia bei ya kuuza na kununua umeme. Anaripoti Jemima Samwel DMC … (endelea).

Wadau muhimu katika kushughulikia bei ya umeme ni Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano tarehe 5 Mei 2021, jijiini Dodoma na Medard Kalemani, Waziri wa Nishati akijibu swali la Ali Hassan Omar, Mbunge wa Jang’ombe visiwani Zanzibar.

Omari alitaka kujua; je, ni lini serikali itatatua mgogoro wa bei ya umeme unaotumika na Watanzania waishio Zanzibar ili kuweka usawa kwa Watanzania wote?

Dk. Medard Kalemani, Waziri wa Nishati

Akijibu swali hilo, Waziri Kalemani amesema, Serikali ya Tanzania na Serikali ya Zanzibar zimeendelea kushughulikia suala la bei ya kuuza na kununua umeme baina ya Tanesco na Zeco ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.

“Katika kipindi cha mwaka 2020/21, timu ya wataalamu wa taasisi husika zilikutana katika vikao mbalimbali, na kufanya uchambuzi wa kina wa vigezo vilivyohusika katika kupanga bei hiyo ya kuuzia umeme kwa wateja wakubwa wa kununua umeme ikiwemo Zeco.

“Kutokana na uchambuzi huo, inapendekezwa kuwa vigezo hivyo vipitiwe upya ili kuleta unafuu kwa wateja wa aina hiyo ikiwemo Zesco,” amesemo na kuongeza:

“Mapendekezo hayo yaliwasilishwa katika kamati ya wizara zinazoshughulikia masuala ya Muungano ili kufanyia kazi mapendekezo hayo na kupata ufumbuzi.”

error: Content is protected !!