Saturday , 10 June 2023
Home Kitengo Michezo Bao Nne za Simba dhidi ya Kaizer, zamuibua Mwigulu adai walikosa mipango
Michezo

Bao Nne za Simba dhidi ya Kaizer, zamuibua Mwigulu adai walikosa mipango

Spread the love

 

WAZIRI wa fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa kilichosababisha klabu ya Simba kukumbana na kadhia ya kipigo cha mabao 4-0, dhidi ya Kaizer chiefs kwenye mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa kulitokana na timu hiyo kukosa mipango. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mwigulu ameyasema hayo leo bungeni, jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitishwa kwa bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Akiongezea jambo mara baada ya kujibu hoja juu ya kodi ya nyasi za bandia, Mwigulu alisema kuwa, katika michezo kuna kitu kinakosewa kwenye mipango, na vitu vingi vinakuja kwa dhararu.

“Kwenye michezo, kuna kitu tunakosea kwenye mipango, vitu vyetu vingi vinakuja kwa dharura.” Alisema Mwigulu

Pia Mwigulu alisema kuwa hata Simba walipopoteza mchezo kule Afrika Kusini dhidi ya Kaizer Chiefs, aliona timu hiyo ilikosa mipango licha ya kuaminishwa kuwa wamehujumiwa.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

“Mimi nilivyoona Simba wamefungwa kule Afrika Kusini na wao wakaaminishwa kama wamehujumiwa na akina Senzo pamoja na watani, mnawalaumu bure.”

“Tunakosa mpango, simba ilienda kucheza Afrika Kusini bila mpango, yenyewe ilijiandaa na mchezo wa watani, na mimi niwapongeze Yanga walikwenda uwanjani wakakaa dakika kadhaa, wakaona Simba hawapo wakaondoka, wakajua wanajiandaa na mchezo.” Alisema Mwigulu

Aidha katika hatua nyingine Waziri huyo aliipongeza klabu ya Simba, kwa kufika hatua kubwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na alitarajia timu hiyo kutwaa kombe hilo, lakini walikosa mipango na kuwataka wanaosimamia mchezo huo kuzipa kipaombele timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa kwa kuwa zinaleta sifa kwa nchi.

“Niwapongeze Simba imefanya hatua kubwa sana, mwaka huu nilivyokuwa naiangalia Simba ya mwaka huu, nilikuwa naiona ya kuchukua ubingwa ila kuna mahali tumekosea kwa sababu hautuweki vipao mbele.”

“Yaani sisi kwetu mambo yote yapo sawa, timu inakwenda kucheza mchezo ambao unaweza kuleta kombe Tanzania ambao ukishinda nusu fainali unaingia fainali, katika yake unaweka mechi ya watani, wanaosimamia watoe kipambele kwa timu hizi, wangeweza kupeleka mchezo mbele.”Alisisitiza Mwigulu

Almas Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB)

Hoja hiyo kutoka kwa Mwigulu imeibuka mara baada ya simba kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya mabingwa dhidi ya kaizer Chiefs kwa jumla ya mabao 4-3, katika michezo yote miwili.

Kabla ya mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ulipigwa Afrika Kusini, Simba ilitakiwa kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga tarehe 8 Mei 2021, na mchezo huo uliahilishwa mara baada ya mabadiliko muda yaliyofanywa na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutoka saa 11 muda uliopangwa awali hadi saa 1 usiku.

Mara baada ya mabadiliko hayo, uomgozi wa klabu ya Yanga hakuliafiki swala hilo na kuingiza timu uwanjani katika muda uliopangwa awali wa Saa 11 jioni.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

error: Content is protected !!