Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Bao la Mkono’ lamtoa chozi Nape 
Habari za SiasaTangulizi

‘Bao la Mkono’ lamtoa chozi Nape 

Spread the love

NAPE Nnauye, Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi sasa anajutia kauli yake ‘bao la mkono’ aliyoitoa miaka minne iliyopita. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea). 

Akizungumza na kituo kimoja cha Runinga hapa nchini tarehe 18 Februari 2019 Nape amesema, kati ya alama atakazokwenda nazo kaburini ni kauli yake ya ‘bao la moko.’

Alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwenye Viwanja vya Nyehunge, Sengerema mkoani Mwanza tarehe 22 Juni 2015. 

Alikuwa katika ziara zilizoandaliwa na Abdurahman Kinana, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ajili ya kukagua utekelezwaji wa Ilani ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.

“Sitaki kujitetea katika hili, ingawa nia yangu haikuwa mbaya. Nami nimeshakubali, kama ni alama iliyo mgongoni kwangu ambayo nitaenda nayo kaburini, ni hii ya bao la mkono,” Nape amesema.

Akionekana kujutia kauli hiyo Nape amesema, kabla ya vyombo vya habari kulishikilia suala hilo, Kinana alimwambia kuwa amekosea na kwamba, ajiandaye kwa tafsiri tofauti kutoka kwa jamii.

“Sikuwa na tafsiri ile, ni kama mpira, hivyo kunaweza kutokea mazingira ya aliyefungwa kutoridhishwa na matokeo ya kufungwa, lakini kama refa hakuona kosa, unabakia kuwa ushindi,” amesema Nape aliyewahi Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na kuongeza;

“Unaposhindana na mtu, anaweza kusogeza kura na kushinda kama mazingira yanaridhisha na katika mataifa makubwa kama Marekani wanafanya hivyo.”

Nape anasema, kauli yake hiyo ilipinduliwa na kutafsiriwa kwamba, CCM ilijipanga kushinda kwa kuiba kura.

Akizungumzia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ‘Bunge Live’ Nape amesema, suala la kusitisha matangazo ya moja kwa moja hakulianzisha yeye bali alisimamia kile alichokikuta wizarani.

Amesema, Shirika la Utangazaji nchini (TBC) lilikuwa likitumia kiasi cha Sh. 4 bilioni kurusha matangazo ya moja kwa moja wakati ambao Bunge lilikuwa na chombo chake cha kurusha matangazo hayo.

“Wapi tulikosea? Tulitakiwa tujadili Kanuni za Bunge ziweje, tukajisahau, tukaanza makelele Nape Nape badala ya kushirikisha wadau wa kutunga kanuni hizo na suala ni nani anarusha ‘live’ (moja kwa moja) au anatakiwa kufanya hivyo, waliotunga kanuni, ndiyo walipaswa kufahamu na kutekeleza hilo,” amesema Nape.

Anakiri kwamba, ushiriki wa wananchi kwa Bunge umeshuka kutokana na kukosa fursa waliyokuwa wakiipata hapo awali.

Hata hivyo ameibua hoja kuwa, kwanini vyombo vya habari vimezuiwa kuweka matangazo kwenye matangazo ya moja kwa moja ya Bunge wakati wanarusha kwa gharama zao binafsi?

Nape akiguzia kutishiwa kwake kwa bastola tarehe 23 Machi  2017 Nape amesema, anajua nani aliyepanga mpango ule na hata walioshiriki, “hata hivyo nimewasamehe.”

Nape alikutwa na mkasa huo wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kutenguwa uteuzi wake katika nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Hata hivyo amesema, hawezi kuwataja waliohusika na kusisitiza waliofanya tukio lile sio watu wa mtaani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!