Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Bao la mkono’ lahojiwa bungeni
Habari za SiasaTangulizi

‘Bao la mkono’ lahojiwa bungeni

Sanduku la kura
Spread the love

WAKATI taifa likijiandaa kuingia kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Oktoba mwaka huu na baadaye Uchaguzi Mkuu 2020, serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), hoja kuhusu ‘bao la mkono’ yaibuliwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wabunge wa upinzani leo tarehe 12 Juni 2019 wametaka kujua, ni kwa namna gani serikali imeandaa mazingira kuhakikisha ‘mchezo’ wa kung’olewa wagombea kwa madai ya kutokidhi vigezo unakoma.

Masoud Abdallah Salim, Mbunge wa Mtambile (CUF) ndiye aliyeibua hilo leo akidai kuwa, ‘mradi’ wa kuwavusha wagombea wa CCM kupita bila kupingwa, umekuwa ikifanywa kwa manufaa ya chama hicho.

Akizungumza bungeni Jijini Dodoma Salim amedai kuwa, kwa sasa kuna hofu na malalamiko makubwa juu ya mbinu chafu zinazotumiwa hivi karibuni, wakati wa zoezi la urudishaji fomu za ushiriki wa uchaguzi wa marudio kwenye maeneo mbalimbali.

Amehoji kuwa, kufuatia changamoto hiyo, serikali haioni kwamba uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2019, hautakuwa wa huru na wa haki?

“Kumekuweko na hofu na malalamiko makubwa juu ya mbinu chafu ambazo zimejitokeza hivi karibuni wakati wa urudishaji fomu, vyama vya upinzani vimekuwa vikiambiwa kwamba, wagombea wao hawana sifa, jambo linaleta hisia mbaya kwamba, CCM inataka ibaki peke yake kwenye uchaguzi.

“Je, huoni mbinu hii chafu ya kuambiwa wapinzani hawana sifa inaweza kusababisha uchaguzi huu kutokuwa huru na haki?” amehoji Salim.

Pia amehoji, kwa nini serikali hanairuhusu CCM kufanya kampeni kabla ya wakati husika, akidai kuwa chama hicho kimeanza kufanya kampeni kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo Morogoro.

Hata hivyo, Mwita Waitara ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi) amekanusha CCM na serikali yake kutumia mbinu chafu na kwamba, Salim ana hofu kuwa katika uchaguzi ujao, wagombea wa chama hicho watachaguliwa wengi kutokana na utendaji kazi mzuri wa Rais John Magufuli.

“Mheshimiwa Masoud anajua watakaochaguliwa wengi ni wa CCM hiyo ndio hofu uliyo nayo, sababu kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli,  miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa. Uwezekano mkubwa wa CCM kupata asilimia 98 ndio unakutisha,” amejibu Waitara.

Aidha, Waitara amesema katika uchaguzi huo hakutakuwa na mbinu chafu kwa kuwa serikali imeandaa utaratibu mzuri wa kutekeleza zoezi la upigaji kura, ikiwemo utaratibu rafiki wa wananchi kujiandikisha, kuhakiki majina yao na wa kupiga kura.

“Hakuna mbinu chafu, utaratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa utatangazwa tarehe na wenye mamlaka, utakuwepo utaratibu wa kujiandikisha kwa muda utakaoatangazwa, yatabandikwa majina kila mtu atahakikisha wakazi na wataenda kwenye kampeni sawa,” amesema Waitara.

Vile vile, Waitara amesema serikali imetenga kiasi cha Sh. 82 Bilioni kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo.

“Ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi serikali imekamilisha kanuni za uchaguzi utakaowezesha kufanyika uchaguzi huo na imetangazwa kwenye gazeti la serikali.  Aidha serikali imehakiki maeneo ya utawala imefanya mafunzo na kutenga Sh. 82 Bilioni kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huo,” amesema Waitara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!