October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Banza Stone afariki dunia

Ramadhan Masanja 'Banza Stone' akiwa jukwaani enzi za uhai wake

Spread the love

MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi, Ramadhan Masanja “Banza Stone” amefariki dunia muda huu nyumbani kwao Sinza. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Kwa mujibu wa ndugu wa Banza, anayefahamika kwa jina la Hamis amelithibitishia Mwanahalisi Online kuwa Banza amefariki dunia mchana huu nyumbani kwao Sinza.

Hamis amesema kuwa hali ya Banza ilibadilika tangu jana usiku, ambapo alikata kauli alikata kauli hadi mchana huu Mungu alipomchukua.

Banza ambaye alitamba na bendi mbalimbali kama African Stars ‘Twanga Pepeta’, Tanzania One Theatre ‘TOT’, Bambino Sound na Extra Bongo, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kifua kikuu na fangasi kichwani kwa muda mrefu.

Mwanahalisi Online itaendelea kuwajuza taratibu za msiba na mazishi.

Inna Lillah Wainna Illah Rajiun 

 

error: Content is protected !!