Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake
Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love

 

SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani Sh. 800 bilioni, ili kutekeleza miradi ya uboreshaji wa bandari zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Lengo la mpango huo, TPA inasema, kunalenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa mizigo na usafirishaji wa abiria nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma, tarehe 2 Juni 2023, Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula, ameeleza kuwa upanuzi na ukarabati wa bandari uliopangwa kufanyika, utasaidia maboresho sekta ya usafirishaji na kuondoa kero kwa wasafiri.

Ametolea mfano wa bandari ya Kigoma, kwamba imewezesha kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam, ambapo hadi kufikia tarehe 31 Mei mwaka huu, imehudumia takribani tani 131,000 za mzigo.

Amesema, idadi hiyo ni sawa na asilimia 48 ya shehena zote zinazohudumiwa katika bandari zote za ukanda wa Ziwa Tanganyika ambapo ni tani 273,000 na kusisitiza kuwa asilimia kubwa ya mizigo inayopitia Dar es Salaam, inasafirishwa kuelekea nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Amesema, “asilimia 80 ya mizigo inayohudumiwa na bandari ya Dar es Salaam, inakwenda DRC); katika mizigo hiyo, asilimia 48 husafirishwa kupitia bandari ya Kigoma.”

Edward Mabula, meneja wa bandari ya Kigoma

Kwa upande wa Ziwa Tanganyika, mamlaka hiyo imewekeza Sh. 100 bilioni, ili kuboresha bandari za ukanda huo, ambazo zimekuwa zikitumika kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kuelekea nchi jirani.

Kutokana na hali hiyo, Mabula ametoa wito kwa wadau wa bandari na sekta binafsi, kuchangamkia fursa zinazotokana na uboreshaji wa bandari za Ziwa Tanganyika.

Kwa upande wake, msimamizi wa mradi wa uboreshaji wa bandari za Kibirizi na Ujiji, Elly Mtaki, ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo, kutaongeza ufanisi katika upakuaji na upakiaji wa mizigo.

“Mamlaka imeamua kujenga gati mpya katika katika bandari ya Kibirizi, ambayo kukamilika kwake, kutaharakisha utoaji wa huduma,” ameeleza Mhandisi Mtaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!