Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bandari bubu 693 zaitesa Serikali
Habari za Siasa

Bandari bubu 693 zaitesa Serikali

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa
Spread the love

 

HATARI za kiulinzi, kiusalama na upotevu wa mapato ya Serikali zimeetajwa kuwa athari za uwepo wa bandari bubu zipatazo 693 nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Athari nyingine ni ushindani usio sawia (unfair competition) baina ya bandari rasmi na zisizo rasmi pamoja na biashara inayofanywa baina ya hizo bandari mbili tofauti.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa leo Jumatatu tarehe 23, Mei 2022 akiwasilisha bajeti ya mwaka 2022/23.

“Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) inatambua changamoto na athari za uwepo wa bandari zisizo rasmi (bandari bubu) katika pwani ya Bahari ya Hindi na kwenye Maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

“Utafiti uliofanyika unaonyesha kwamba hadi Juni, 2021 kulikuwa na jumla ya Bandari zisizo rasmi 693.”
Mbarawa amesema kati ya hizo, bandari 239 ziko katika mwambao wa bahari ya Hindi, bandari 329 katika Ziwa Victoria, bandari 108 katika Ziwa Tanganyika, na bandari 17 katika Ziwa Nyasa.

Waziri huyo ameongeza kuwa wizara kwa kushirikiana na TAMISEMI imezielekeza Taasisi zinazohusika na suala hilo kuendelea na zoezi la kutathmini bandari zisizo rasmi ili kuishauri Serikali kuzirasimisha kwa lengo la kuimarisha usalama, kuongeza fursa za ajira na mapato ya Serikali.

Amesema hadi Aprili 2022, jumla ya bandari zisizo rasmi 20 zilikuwa zimeainishwa katika awamu ya kwanza kwa ajili ya kuzifanyia tathmini ya kina ili kuzirasimisha.

1 Comment

  • Duh!
    Tungeni sheria. Maneno matupu hayavunji mfupa. Angalau sheria zingekuwepo haya malalamiko yasingetokea.
    Kwanini mnasubiri shida itokee ndipo mlalamike. Kama sheria zingekuwepo hatua kali zingechukuliwa na kusingekuwa na bandari bubu zinazotorosha madini yetu, na kuingiza vitu toka China, Pakistani na India bila kulipia ushuru.
    Miambao yote ya bahari, maziwa na visiwa pia iwekewe zuio kujengwa au kuchimbwa kabla ya kupatiwa ripoti ya faida na athari za mazingira husika yakibadilishwa.
    Je, tunahitaji vitabu vya sheria za nchi zingine kujifunza?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!