January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Banda awagawa viongozi Simba

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Simba pamoja na benchi la ufundi kwa sasa wapo katika wakati mgumu juu ya kuamua hatma ya mkataba wa kinda Peter Banda raia wa Malawi kama atasalia klabuni hapo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Awali mchezaji huyo alikuwepo kwenye orodha ya wachezaji wanne wa kigeni ambao watavunjiwa mikataba yao au kutolewa kwa mkopo kwenye dirisha hili dogo la usajili kufuartia kutopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hiko cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Banda alisajiliwa kwenye dirisha kubwa kla usajili mwezi Agosti, 2021 na kupewa matumani makubwa ya kufanya vizuri kwenye kikosi cha Simba kiasi cha baadhi ya watu kuamini kuwa, kinda huyo atakuwa mrithi sahihi wa Luis Miquisone aliyetimka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Al Ahly ya nchini Misri.

Taarifa za kuaminika kutoka kwenye chanzo ndani ya klabu ya Simba kinaeleza kuwa, baadhi ya viongozi wameoneka  kutokubaliana na suala la kuvunjiwa mkataba au kutolewa kwa mkopo kwa mchezaji huyo mara baada ya kuonekana kufanya vizuri mazoezini katika siku za hivi karibuni.

Mchezaji huyo ambaye amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinachokwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa Afrika Januari 2022 nchini Cameroon.

Tayari mpaka sasa uongozi wa klabu hiyo umeshafikia muafaka wa kuvunja mkataba na wachezaji Pascal Wawa pamoja na Duncan Nyoni Raia wa Malawi.

Uongozi wa Simba umeamua kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao kwa ajili ya kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika hayo yote yanayoendelea ikumbukwe siku ya jana Klabu ya Simba ilitangaza kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili na kiungo mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu ambaye ametimkia klabu ya Azam FC.

Sambamba na hilo pia klabu ya Simba siku za hivi karibuni ilifikia tamati ya kuvunja mkataba na kocha wake msaidizi Raia wa Rwanda Thierry Hitimana.

error: Content is protected !!