August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ban  Ki Moon apata mrithi UN

Ban Ki Moon, Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa UN

Spread the love

ANTONIO Manuel de Guterres, Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno na Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kitengo cha kuhudumia wakimbizi ndiye Katibu Mkuu Mpya wa Umoja Mataifa (UN), anaandika Wolfram Mwalongo.

Guterres (68), alikuwa Waziri Mkuu wa Ureno (1995 – 2002) na ameshikilia nafasi ya ukurugenzi katika ofisi za UN akishughulikia wakimbizi tangu Juni 2005 hadi 2015 lakini pia anasifika kama mwanadiplomasia mashuhuri duniani.

Sherehe za kuchaguliwa kwa kwa Guterres na kumuaga Ban Ki Moon aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN zimefanyika katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York  Marekani, ingawa Guterres anatarajia kuanza kazi Januari mwakani.

“Tunaamini Guterres ataiongoza UN kwa hekima na uadilifu,” amesema John William Ashe ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la UN.

Guterres ameeleza malengo yake akisema “mwisho wa vita baridi umezaa vita vya kale, UN ilizaliwa kutokana na vita na leo lazima kuwa hapa kwa amani.”

Aidha amesisitiza jambo la usawa wa kijinsia kuwa kipaumbele chini ya utawala wake ndani ya UN katika ngazi zote kutoka juu hadi chini.

Wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanadai kuwa huenda Guterres akamteua Bi. Amina Mohammed, Waziri wa Mazingira wa Nigeria kuwa naibu wake.

Guterres ameongeza kuwa kutokanana na migogoro iliyopo katika nchi mbalimbali duniani nivema kukawepo na ubunifu katika diplomasia ili kusaidia kushawishi  na upatanishi katika mataifa hayo.

“Kutokana na migogoro iliyopo katika nchi za Syria, Yemen, Sudan Kusini na maeneo mengine, Pia ile ya muda mrefu kama Israel na Palestina diplomasia ya ubunifu inahitajikaili kushawishi na kupatanisha na pale patakapohitaji nguvu  binafsi nitajitahidi kuongeza shinikizo,” amesisitiza.

error: Content is protected !!