Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Balozi wa Poland aongoza kusafisha ufukwe Kawe
Habari Mchanganyiko

Balozi wa Poland aongoza kusafisha ufukwe Kawe

Spread the love

KRZYSZTOF Buzalski, Balozi wa Poland nchini Tanzania ameungana na wadau wa masuala ya usafi, kusafisha ufukwe wa Kawe jijini Dar es Dalaam. Anaripoti Brightness Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Usafi huo umefanyika leo Jumatatu tarehe 21 Septemba 2020.

Mara baada ya kukamilisha shughuli hiyo, Balozi Buzalski amesema, amefurahishwa kushirikiana na Watanzania waliojitokeza kufanya usafi kwa sababu tatizo likitokea la uharibifu wa mazingira litaathiri watu wote.

Amesema, suala la taka za plastiki zipo kila sehemu na anafurahi kuona kila mwaka watu wakijitokeza kufanya usafi hivyo kila mmoja asimame katika nafasi yake kuzuia uchafuzi katika fukwe.

“Nimefurahi kuona Watanzania na wageni ambao wamejitokeza kufanya usafi kwa pamoja, kwa sababu tatizo tunalo kumbana nalo linaenda kutuadhiri wote, haijalishi unaishi Ulaya, Tanzania au Australia.”

“Uchafu wa plastiki upo kila mahali, kwa hiyo ninafuraha kila mwaka kuna kundi dogo la watu wanaoamu kuchukua nafasi katika shughuli ya usafi,” amesema Balozi Buzalski

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!