Monday , 22 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi CCM akamatwa na bangi
Habari za SiasaTangulizi

Balozi CCM akamatwa na bangi

Viroba vilivyosheheni bangi
Spread the love

BALOZI wa nyumba kumi mkazi wa Kasumulu wilayani Kyela mkoa wa Mbeya, Andende Smoke Mbalwa (35) pamoja na Rose Charles (40) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kutokana na tuhuma za kukutwa na debe tatu za bangi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za tukio hilo zimetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP, Ulrich Matei, ambapo amesema watuhumiwa hao walinaswa katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo.

Kamanda Matei amedai kuwa, Mbalwa na Charles ni wauzaji na watumiaji wa bangi hiyo. Na kwamba upelelezi dhidi yao unaendelea na watafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika.

Katika hatua nyingie, Kamanda Matei amesema Polisi wanawashikilia watu watatu, Okoka Sanga (48) mkazi wa Ushirika Tukuyu, Festo Hassan (25) na Cosmas Ngondo (33) mkazi wa kijiji cha Lema wilayani Kyela, kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumchoma kisu sehemu za shingoni Elizabeth Mwampamba (44) mkazi wa Stamiko.

“Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 1Oktoba 2018 majira ya saa 00:05 usiku huko Kijiji cha Stamiko kilichopo Kata ya Busale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Elizabeth Mwampamba akiwa amelala nyumbani kwake ambapo anaishi na watoto wake, alivamiwa na mtu/watu wasiofahamika na kisha kuchomwa kisu sehemu za shingoni,” amesema Kamanda Matei.

Kamanda Matei amesema Mhanga wa tukio hilo amelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Wakati polisi wakiendelea na upelelezi kubaini chanzo cha tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!