Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Balozi: Palestina haitalegeza kamba
Habari Mchanganyiko

Balozi: Palestina haitalegeza kamba

Spread the love

TAIFA la Israel limeondoa furaha yetu, linataka kuondoa utambulisho wetu katika ardhi ya Palestina, kamwe hilo halitafanikiwa. Anaandika Yusuph Katimba…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 10 Oktoba 2018 na Hamdi Mansour AbduAli, Balozi wa Palestina nchini Tanzania alipoulizwa na wanahabari kuhusu kinachoendelea kwenye mgogoro wa taifa lake na Israel.

Akiwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam AbduAli amesema, uhalali wa Palestina katika ardhi yake ni jambo linalofahamika ulimwenguni na kinachafanywa na Israel dhidi ya Palestina hakitarudisha juhudi za kutetea ardhi yao.

“Wapalestina wanataabika kutokana na Israel kuondoa furaha yetu. Juhudi za kutatua mgogoro zinashindikana kufikiwa kutokana na Israel kushindwa kuheshimu makubaliano ya Umoja wa Mataifa (UN),” amesema AbduAli akisitiza Palestina itaendelea kupigania utambulisho wake.

AbduAli amesema, yapo mambo yanayoonesha kuwa wanaosimamia mazungumzo ya muafaka hawalengi kupata muafaka wa mgogoro wa Palestina na Israel kwa sababu ya kuubeba upande mmoja na kisha kuukandamiza upande mwingine.

“Angalia namna Marekani ambaye ndio msuluhishi, anachukua ardhi ya Wapalestina (Jerusalem) na kuwakabidhi Israel halafu hapo hapo anakwita kwenye meza ya mazungumzo. Unawezaje kumwamini mtu wa namna hii?” amehoji AbduAli.

Balozi huyo amesema kuwa, Palestina haiwezi kuingia kwenye makubaliano yanayoweza kuangamiza ama kuumiza taifa hilo na kwamba, makosa ya Israel na Marekani hayawezi kusahihishwa na Palestina.

Akizungumzia ushirikiano wake na Tanzania AbduAli amesema kuwa, Serikali ya Rais John Magufuli ina ushirikiano mzuri na Palestina.

Kutokana na hali hiyo Palestina itaendelea kushawishi wafanyabiashara wa taifa hilo kuendelea kuwekeza Tanzania kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Rais Magufuli anashirikiana vizuri na Palestina nasi tutaendelea kushirikiana na Tanzania katika mambo mbalimbali ili kuboresha ushirikiano,”amesema AbduAli.

Palestina hivi karibuni imeingia kwenye makubaliano na masuala ya Utalii na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambapo ameeleza kuwa, mpango wa kuwekeza kwenye Utalii kwa upande wa Tanzania bara unaendelea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!