April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Balozi Palestina aingia kwenye mapambano dhidi ya corona

Spread the love

KATIKA kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19), Serikali ya Palestina imepanga kuikabidhi serikali mashine ya kutakatisha mwili (sanitization machine). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia makabidhiano hayo, Hamdi Mansour AbuAli, Balozi wa Palestina nchini Tanzania amesema, taratibu za makabidhiano zinafanywa kati ya Serikali ya Palestina na Tanzania.

Amesema, msukumo wa utoaji msaada hiyo unatokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali ya Tanzania na Palestina, huku akisisitiza mampambano dhidi ya corona kwamba ni muhimu.

“Katika azma ya kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kukabili changamoto ya kihistoria iliyoletwa na janga la corona.

“Serikali ya Palestina imeishaandaa msaada wa machine ya maji tiba (sanitization machine) kwa serikali ya Tanzania, yenye uwezo wa kusafisha mwili mzima wa mtu,” amesema AbuAli na kuongeza:

“Mashine hii imetengenezwa hapa hapa nchini kwa ushirikiano kati ya Mhandisi wa Palestina na wataalamu wa Tanzania.”

Balozi AbuAli amesema, mashine hiyo ni rahisi kuitumia na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

Amesema “ingawa Palestina ina rasilimali chache, imedhamiria kuungana na serikali ya Tanzania kwenye vita dhidi ya corona.”

error: Content is protected !!