July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Balozi Mulamula apokea hati za Balozi Japan

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Japan nchini, Misawa Yasushi leo tarehe 20 Juni, 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akipokea nakala ya hati hizo, Balozi Mulamula amemhakikishia Balozi huyo mteule ushirikiano wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.

Naye Balozi Mteule wa Japan nchini, Misawa Yasushi amesema atahakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Japan unaimarika zaidi na kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizi kupitia nyanja za biashara na uwekezaji na hivyo kunufaisha pande zote mbili.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa China anayeshughulikia masuala ya Afrika, Wu Peng.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula na mgeni wake, walijadili namna ya kuendelea kuimarisha maeneo ya ushirikiano katika sekta za afya, elimu, bishara na uwekezaji, nishati, miundombinu na usafirishaji.

error: Content is protected !!