Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Balozi aliyeuawa Congo, mwili warejeshwa Roma
Kimataifa

Balozi aliyeuawa Congo, mwili warejeshwa Roma

Spread the love

 

MWILI wa Luca Attanasio, aliyekuwa Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), umerejeshwa Roma nchini humo kwa ajili ya maziko. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kundi la waasi, DRC lilivamia na kushambulia magari ya Umoja wa Mataifa (UN), ambapo kwenye msafara huo, alikuwemo balozi huo.

Tukio hilo lililosababisha kifo cha Attanasio, mlizi wake Vittorio Lacovacci na dereva wake, raia wa DRC aliyetajwa kwa jina la Moustapha Milambo, lilitokea juzi Jumatatu tarehe 22 Februari 2021.

Magari hayo ya UN, yanaelezwa kwamba yalikuwa yamebeba chakula cha msaada. Mashambulizi hayo yalitokea Goma, mashariki mwa nchi hiyo.

Waasi hao walipanga kuteka nyara magari hayo na mali zote, hata hivyo hawakufanikiwa.

Mwili wa balozi huyo sambamba na wa mlinzi wake, ulisafirishwa kwa ndege ya Jeshi la Italia.

Miili hiyo iliokuwa imefunikwa kwa kitambaa cha bendera ya taifa hilo, ilipokewa katika Uwanja wa Ndege wa Ciampino na Waziri Mkuu, Mario Draghi.

Serikali ya DRC, imeelekeza tuhuma na lawama zake kwa kundi la waasi wa Rwanda, FDLR kwamba ndio lililohusika kwenye mauaji hayo. Hata hivyo, FDLR limekanusha kuhusika na shambulio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Makamu Rais Malawi, wengine 9 wafariki kwa ajali ya ndege

Spread the loveMakamu wa Rais wa Malawi, Saulos Chilima pamoja na watu...

error: Content is protected !!