Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAKWATA yatikiswa bungeni
Habari za SiasaTangulizi

BAKWATA yatikiswa bungeni

Baadhi ya wabunge wa Upinzani katika Bunge lililopita
Spread the love

MBUNGE wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea, amehoji hatua ya serikali ya kulipa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia, Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza bungeni mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu leo Jumatatu, tarehe 7 Mei, Kubenea amesema, “serikali imetoa mamlaka ya mwisho ya kupeleka mahujaji nchini Saudia Bakwata ili kutimiza nguzo kuu ya uislamu.”

Amesema, “jambo hili ni kinyume na Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hatua hii, ni kinyume na sheria za nchi na kinyume na matakwa ya uislamu na waislamu.

“Hivyo basi, kwa kuwa Bunge ndio chombo kikuu cha wananchi kwa mujibu wa Katiba; chombo hiki kwa mujibu wa Katiba, ndicho kinachosimamia serikali na kuishauri kwa niaba ya wananchi, naomba serikali itueleze kwa nini imetoa mamlaka haya kwa BAKWATA, wakati chombo hiki siyo mali ya waislamu wote?”

Akizungumza kwa hisia kali, Kubenea alisema, “Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inatamka kuwa serikali haina dini. Lakini serikali hii, imejiingiza kwenye mambo ya dini na kutaka waislamu wote kwenda Hijja kupitia Bakwata.”

Amesema, “taifa hili lina taasisi 11 zenye usajili sawa kama Bakwata. Kuwalazimisha waislamu wote kutumia Bakwata kwenye mambo ya Hijja, ni kinyume na katiba. Haikubariki.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

error: Content is protected !!