BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kuwa, tarehe 12 Septemba mwaka huu ni siku ya Sikukuu ya Eid el Hajj, anaandika Aisha Amran.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Salim Abeid mwakilishi wake amesema, Sikukuu ya Eid kitaifa itaadhimishwa jijini Dar es Saalam na kuswaliwa katika Viwanja vya Bakwata.
Amesema, Baraza la Eid litafanyika baada ya Swala ya Eid na mgeni rasmi atakuwa Sheikh Abubakar Zubeir, Mufti Mkuu wa Tanzania.
More Stories
Exim waadhimisha miaka 25, yapongeza wafanyakazi wake
NMB yamwaga vitanda, magodoro Kagera
NBC wasisitiza kukuza michezo, sanaa na utamaduni