January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti yapondwa kona zote

Begi la lililobeba bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16

Spread the love

BAADHI ya wasomi wamesema Bajeti ya Serikali ya Sh. 22.4 trilioni kwa mwaka 2015/16, iliyosomwa jana bungeni, haina nia ya kuwakomboa Watanzania katika dimbwi la umasikini. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mbali na kuwasaidia watanzania pia, wafanyakazi nao wamesema kuwa kile kilichoonekana kuongezwa katika mshahara ni kiini macho kwani maisha yataendelea kuwa magumu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya za wanataaluma Tanzania, Poul Loisulie alipokuwa akizungungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum juu ya mwonekano wa bajeti iliyosomwa bungeni.

“Binafsi naitazama bajeti ya mwaka huu kwa sura mbili, kwanza kabisa ni bajeti ya uchaguzi, makusanyo kwa sehemu kubwa yataelekezwa kwa uchaguzi wa mwaka huu.Hata wabunge wenyewe hawana hamu kubwa ya kujadili bajeti wala kuichambua kwani hawategemei kitu chochote kipya.

“Pili kupandishwa kwa gharama ya mafuta ya petrol, dizel na mafuta ya taa itasababisha kuvurugika kwa mfumo mzima wa uchumi wa maisha. Kwa sisi wafanyakazi hata kama mshahara wa mfanyakazi utapanda, kiasi chote cha nyongeza hakitaingia mfukoni mwake bali italipia gharama iliyoongezeka,”amesema.

Amefafanua kuwa, hilo litakuwa tatizo kwa jamii yote kwa makundi yote, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa watanzania kuendelea kuwa masikini.

Kwa upande wake, mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Mtawala wa mambo ya fedha, Aulelius Lema, amesema  kwa ujumla bajeti ya mwaka hii haina jambo jipya bali itaongeza mfumko wa bei.

Amesema kitendo cha kuwepo kwa ongezeko la mafuta kitasababisha kila kitu kupanda bei.

“Bajeti siyo halisi, ukiongeza kodi katika mafuta ya Petrol, Dizel na mafuta ya taa ni wazi kuwa unaendelea kukaribisha uharibifu wa mazingira.Hata kama kweli hizo fedha za mafuta zikipelekwa REA ni wazi kuwa haziwezi kufanya kazi iliyokusudiwa na wananchi hawawezi kupata nishati ya umeme kwa wakati,”amesema.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Caberisa Kampany Ltd iliyopo Mpwapwa, mhandisi Benard Mgoha, akizungumzia kupandishwa kwa mafuta, amesema serikali imetafuta njia mbadala ya kuwafanya watanzania wengi kuozea mahabusu.

Amesema kamwe haiwezekani serikali kuweka sera ya kutunza mazingira huku ikipandisha bei ya mafuta na kwa kufanya hivyo ni dalili za kuwakomoa watanzania na kuwataka waendele kufa na umasikini.

“Tunasema kwa sasa tunapambana na utunzaji wa mazingira ni lazima tuwawezeshe watanzania kutumia nishati mbadala kama bile umeme, gesi na mafuta.

“Ninaishangaa serikali sijui inashauriwa na nani, bajeti ya mwaka huu ni mbaya ambayo haijawai kutokea kwani imelenga kuwadhoofisha watanzania wote,” amesema  

error: Content is protected !!