Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa BAJETI YA SERIKALI: Kitanzi kingine kipya chaja  
Habari za SiasaTangulizi

BAJETI YA SERIKALI: Kitanzi kingine kipya chaja  

Dk. Philip Mpango, wakati akiwa Waziri wa Fedha na Mipango 2015-19
Spread the love

KODI! Kodi! Kodi, ndio mwelekeo wa Bajeti ya ya nne tangu Rais John Pombe Magufuli ashike madaraka, akiwa na kauli tamu na ahadi kedekede zikiwamo, “Tanzania ya viwanda.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Baada ya kulaumiwa na wanauchumi nchini na hata wafadhili kufikia hatua ya kukata sehemu ya misaada yao, sasa serikali imekuja na “panga la kodi.”

Miongoni mwa maeneo ambayo yanatajwa kupewa kipaumbele cha kuwekewa mkwazo kwenye kodi, ni pamoja na “kiunua mgongo cha wabunge, vinywaji baridi, ikiwamo soda na maji; bia na mafuta ya magari na mafuta ya taa.”

Aidha, maeneo mengine ambako kodi itauma ni pamoja na pale ambako kulikuwa na misamaha ya kodi na kwenye bidhaa ambazo serikali imejenga utamaduni wa kupandisha bei zake kila mwaka.

Asubuhi hii, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philiph Mpango amewasilisha mpango wa serial katika mwaka wa fedha ujao. Katika hotuba yake, Dk. Mpango alidai kuwa katika kipindi cha maka mitatu iliyopita, hali ya uchumi imezidi kuimarika na uchumi wa taifa umekuwa kwa asilimia 7.5.

Nyaraka nyingine za serikali ambazo MwanaHALISI Online limeziona, vinathibitisha mwelekeo wa ongezeko la vyanzo vya kodi na kodi yenyewe.

Dk. Mpango aliiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, wiki iliyopita kuwa serikali inaimarisha mfumo wa makusanyo yake ya kodi kwa kuhusisha vyanzo vipya.

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, serikali inatarajiwa kutumia Sh. 33 trilioni, kutoka kiasi Sh. 32 trilioni zilizotengwa katika bajeti ya mwaka jana.

Bajeti ya sasa inakuja wakati serikali ya Rais Magufuli inalaumiwa kwa kuzorotesha uchumi na kushindwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara nchini.

Dk. Mpango anatarajiwa kulieleza bunge pigo lililoipata serikali kutokana na kushuka kwa kiwango cha mikopo kutoka nchi wahisani na marafiki wengine.

Katika kile alichoita, “Mfumo wa Mapato na Matumizi ya Serikali,” Dk. Mpango ameweka mwelekeo wa bajeti katika kukusanya mapato ya ndani; kuzingatia kwa makini vipaumbele vilivyoanishwa kupitia mchakato wa MKUKUTA, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya 2015 na Malengo ya Milenia

Maeneo mengine, ni kutekeleza bajeti ya maendeleo kwa kutoa umuhimu wa kwanza katika kulipa madeni ya mikataba ya ujenzi na kukamilisha miradi inayoendelea, hususani ya miundombinu na maji.

Kama huu ndio mwelekeo wa bajeti ya serikali, wananchi wasitarajie miujuza. Bajeti ya Dk. Mpango haina kipya. Ni bajeti iliyoandaliwa kisiasa, iliyojaa mipango isiyotekelezeka na inayojikanganya kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!