March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti ya Lukuvi yapita bungeni

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi

Spread the love

JANA serikali ilpitisha bajeti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya mwaka wa fedha 2018/19 kiasi cha Sh. 73,071,273,638. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Pamoja na kupitisha bajeti hiyo lakini bado wabunge wamesema kuwa wanakerwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa wizara hiyo hususani waliopo katika halmashauri kuzalisha migogoro ya ardhi.

Akichangia hoja wakati wa upitishwaji wa bajeti ya Wizara hiyo Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), amesema kuwa licha ya Waziri Lukuvi kutatua mzozo wa eneo la hekali 400 kisha kuzirudisha serikali, lakini baadhi ya viongozi wa mkoa wa Lindi, hawajapendezewa na uamuzi huo.

Amesema eneo hilo limekwisha amriwa kurudishwa kwa wananachi lakini bado aliyekuwa mmiliki amegoma kutoa funguo za zahanati iliyokwisha jengwa ili wananchi waanze kuitumia.

Kwa sababu hiyo, alimuomba Waziri Lukuvi kutoa agizo hilo kwa mara nyingine ikiwo kuandika barua kwa viongozi wa mkoa huo ili wamshinikize mwekezaji kutoa funguo za zahanati.

Kadhalika, Mbunge wa kuteuliwa Anne Kilango Malecela (CCM) , amemuomba Lukuvi kufika wilaya ya Same kwenye Kata za Makanya na Ndugu, kushuhudia uhaba wa ardhi unaowakabili wakazi wa kata hizo.

Amesema maeneo makubwa ya kata hizo ni mashamba ya mkonge ambayo hayana tija kwa wananchi hivyo ni muhimu yakarejeshwa kwao wayatumie kwa shughuli za kiuchumi.

Akijibu hoja hizo, Waziri Lukuvi amesema maoni yote ya wabunge yatazingatiwa ili kuongeza juhudi za kuwahudumia wananchi.

Pia aliagiza Shirika la Nyumba (NHC) kukutana na chama cha wapangaji ili kutatua mgogoro uliopo baina yao.

Akijibu hoja ya Bobali, amesema eneo hilo lililolejeshwa serikali ni yakisheria hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, wanapaswa kufahamu ni eneo la kisheria.

“Hili hatubabaishani ndani ya serikali na zile zahanati zinafunguliwa. Nashangaa nani anayegoma kufungua zile zahanati manasubili nani awafungile..? Nitarudi Lindi na Mtwara kupambana na huyu tapeli ambaye amekuwa akiwanyanyasa wananchi,” amesema.

Lukuvi pia amesema kulikuwa na tatizo kwa baadhi ya maofisa ardhi wakishapewa rushwa, wanabadili mpaka lakini sasa mipaka yote itarekebishwa.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Wizara hiyo imekuwa ya pekee ambayo hakuna chama chochote kilichowasilisha kuzuia mshahara wa waziri wakati bunge lilipokaa kama kamati.

error: Content is protected !!