Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bajeti ya Kilimo yamkuna Mbunge Ditopile, ampongeza Rais Samia
Habari za Siasa

Bajeti ya Kilimo yamkuna Mbunge Ditopile, ampongeza Rais Samia

Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Mariam Ditopile
Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Mariam Ditopile ameimpongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti ya kilimo inayokwenda kufanya mapinduzi kwenye sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ditopile amesema hayo leo Jumatano tarehe 17 Mei 2022, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo yam waka 2022/23 ya Sh.751.12 bilioni ikiwa imeongezeka kutoka Sh.294.16 bilioni.

Bajeti hiyo iliwasilishwa jana Jumanne na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 155.34 ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na miundombinu ya uhifadhi wa mazao.

Pia, kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao, kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu na utoaji wa ruzuku.

Akichangia bajeti hiyo, Ditopile amesema, kwa kipindi kirefu bajeti ya kilimo imekuwa ikilalamikiwa na wabunge kwamba ni kidogo lakini mwaka huu imepanda huku akimpongeza Rais Samia kwa kuwateua Bashe kuwa waziri na Anthony Mavumbe kuwa naibu ambao wanaonesha mwanga kwenye sekta hiyo.

“Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kwenye nchi yetu hii ni bajeti ya kwanza inaletwa na Serikali na hakuna mtu analalamika kwamba ni ndogo hapa nimpe pongezi Rais Samia Suluhu Hassan kwa hakika ameonesha yeye ni mkulima mwenzetu na anajali kwa vitendo maslahi ya wakulima nchini na hilo amedhihirisha kwa kutuletea waziri na naibu wake wenye kujali wakulima,” amesema Ditopile.

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo

Amesema, “kilimo kinafanyika sana nchini, ndio maana katika takwimu za Serikali tunaelezwa kilimo kimeajiri asilimia kubwa ya Watanzania, lakini cha kushangaza mkulima anakutana na serikali baada ya kuvuna.”

“Kilimo ni utafiti na utaalamu, ni udongo ama mbegu, ni sayansi na teknolojia, ni dawa, ni maji kwa maana ya mvua au umwagiliaji, ni miundombinu ya uvunaji, ni urutubisho, ni uhifadhi na ni soko na ukikosoea jambo moja umeondoa tija kwenye kilimo,” amesema

Mbunge huyo kutoka Mkoa wa Dodoma amesema, “tusiache sayansi na teknolojia, twende sawa na dunia, kwa nini tunakataa mbegu za GMO, tunazikataa kwa nini, tunalima Pamba tunataka kuzalisha nguo, lakini Brazili, India na China wanatumia GMO, sisi tunachokitaka tuleteeni na mkulima aamue, mnasema zina madhara ni uongo mtupu.”

Aidha, Ditopile amezishauri wizara ya kilimo kufanya kazi kwa ukaribu na wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara ili kuwezesha kuwasaidia wakulima kulima mazao yenye tija kwa kipindi fulani.

“Nishauri kwamba, tuanzie sokoni, leo hii uhaba wa mafuta ya kula umekuja kujulikana kupitia viwanda vya kibiashara. Niombe wizara ya kilimo na ya biashara mkae pamoja na kushirikiana ili kuwashauri wakulima walime mazao gani yenye tija kwa musimu husikakuwa,” amesema Ditopile na kuongeza:

“Bajeti ya kilimo imepanda, niliwahi kushauri vijana lazima watengenezewe namna ya kushiriki kwenye kilimo, naona kundi kubwa hili ambalo nimekuwa mtetezi wao mmewakumbuka na mnakwenda kutoa vitendea kazi na watashiriki sasa kwenye kilimo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!