SERIKALI imetekeleza bajeti ya miradi ya maendeleo sekta ya ujenzi kwa asilimia 96.5 kwa yenye gharama ya Sh. 1.532 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Hayo yamebainishwa leo Jumatatu tarehe 23 Mei, 2022 na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha bajeti yam waka 2022/23.
Mbarawa amesema hadi Aprili, 2022 fedha zilizopokelewa ni Sh. 1.532 sawa na asilimia 96.48 ya fedha zilizoidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/22. Sekta ya Ujenzi ilitengewa Sh 1.588 trilioni ikijumuisha Sh 1.288 fedha za ndani na Sh 300 milioni fedha za nje.
Amesema kati ya fedha zilizopokelewa Sh 1.232 trilioni ni fedha za ndani zinajumuisha Sh 691.1 milioni kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na Sh. 541.6 milioni kutoka Mfuko wa Barabara na Sh 299.9 milioni ni fedha za nje.
Leave a comment