May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti 2021/22: Washindi wa michezo ya kubahatisha kucheka

Spread the love

WAZIRI wa fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema kuwa kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22 serikali itapunguza kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Gaming tax on Winning) kwa asilimia tano. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwigulu ameyasema hay oleo Bungeni tarehe 10 Juni, 2021 wakati alipokuwa akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Katika wasilisho hilo Waziri huyo alisema kuwa anapenda kufanya mabadiliko katika sharia ya michezo ya kubatisha, sura 42 kwa kupunguza kiwango hiko kwa zawadi ya mshindi kutoka asilimia 20 hadi asilimia 15.

“Mheshimiwa Spika napenda Kupunguza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi (Gaming tax on Winnings) kutoka asilimia 20 hadi asilimia 15.” Alisema Mwigulu

Aidha katika hatua nyingine Waziri huyo alipendekeza ongezeko la kodi katika michezo ya kubatisha ya ubashiri wa matokeo ya michezo kwa mapato ghafi kutoka asilimia 25 ya mauzo ghafi hadi asilimia 30 ya mauzo ghafi.

“Kuongeza kiwango cha Kodi katika michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo ya michezo (sports betting) kwa mapato ghafi (Gross Gaming Revenue – GGR) kutoka asilimia 25 ya mauzo ghafi hadi asilimia 30 ya mauzo ghafi.” Aliongezea Mwigulu

Serikali ilifafanua kuwa lengo la ongezeko hilo la kodi, zitasaidia katika maendeleao ya michezo, katika ongezeko la asilimia 5.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Pia Waziri huyo alitoza kodi ya michezo ya kubahatisha kwa asilimia 10 ya mapato ghafi kwenye michezo ya kubahatisha inayoendeshwa kwa kompyuta.

Mwigulu alifafanua kuwa lengo la marekebisho hayo zitaweza kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi cha shilingi 14,925.38. Mil

error: Content is protected !!