Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bajeti 2019/20 yasheheni mipango lukuki
Habari Mchanganyiko

Bajeti 2019/20 yasheheni mipango lukuki

Dk. Philip Mpango
Spread the love

KATIKA mwaka wa fedha wa 2019/20 Serikali inakusudia kutumia bajeti ya shilingi tilioni 33,105.4 tofauti na bajeti mwaka wa fedha wa 2018/19 ambayo ilikuwa ni Sh. tirioni 32,476. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Sambamba na hilo, vipaumbele vilivyopendekezwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2019/20 ni vinne wakati vipaumbele vya mwaka wa fedha 2018/19 vilikuwa 25.

Kwa mujibu wa maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akiwasilisha mapendekezo ya serikali  ya mpango wa maendeleo wa taifa na ya kiwango cha ukomo wa Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha kwa mwaka wa fedha 2019/20 amesema kuwa, serikali inakusudia kutumia kiasi cha Sh. Tilioni 33,105.4.

Dk. Mpango amesema kuwa, kuzingatia sera ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20 sura ya bajeti inaonesha kuwa, jumla ya sh. Bilioni 33.105.4 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika ambapo mapato ya ndani yakijumuisha mapato ya halmashauri yanatalajiwa kuwa sh. tilioni 23,045.3.

Amesema, mikopo ya ndani inakadiriwa kuwa sh.tilioni 4,960 mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara itakuwa sh. Tirioni 2,316.4 na misaada na mikopo yenye masharti nafuu kutoka kwa washirika wa maendeleo sh.tirioni 2,783.7.

Waziri huyo amesema, katika fedha hizo zinajumuisha matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo na kuwa, kati ya fedha hizo sh.trion 20,856.8 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo matumizi hayo yanajumuisha gharama za uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Aidha alieleza kuwa, matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa sh.tirioni 12,248.6 ambapo sh.tirioni 9,737.7 ni fedha za ndani na tirioni 2,510.9 ni fedha za nje.

Akiwasilisha mapendekezo hayo Dk. Mpango amesema kuwa, katika kutekeleza bajeti vipo vipaumbele vinne.

Alivitaja hivyo kuwa ni viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda ambapo miradi itakayo tekelezwa katika eneo hilo ni ile yenye lengo la kujenga viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini hususani kilimo, madini na gesi asilia.

Amesema kuwa, miradi hiyo ni pamoja na kiwanda cha kuchakata gesi asilia, uanzishwaji na uendelezaji wa kanda maalum za kiuchumi na kongani za viwanda, vya kuongeza thamani maazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, kuongeza thamani ya madini na usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu.

Kipaumbele kingine alikitaja kuwa ni kufungamanisha ukuaji wa uchumi na maenddeleo ya watu ambapo miradi itakayotekelezwa katika eneo hilo ni ile yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, elimu na ujuzi, upatikanaji wa chakula na lishe bora pamoja na huduma za maji safi na salama.

“Shughuli zitakazotiliwa mkazo ni pamoja na kugharamia utoaji wa elimu msingi bila ada, kupunguza vifo kwa akina mama vinavyotokana na uzazi, utekelezaji wa program ya maendeleo ya sekta ya elimu (Programu ya lipa kulingana na matokeo katika elimu),ujenzi wa ukarabati wa vyuo vya ufundi stadi nchini ,kuboresha huduma za maji vijijini,” amesema Mpango.

Pamoja na hayo ametaja kipaumbele kingine kuwa ni uboreshaji wa mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji.

Hata hivyo amesema, miradi itakayotekelezwa katika eneo hilo ni ile yenye lengo la kuendeleza ujenzi na ukarabati wa miundombinu (Reli,bandari,nishati,viwanja vya ndege na barabara).

Miradi hiyo ni pamoja na miradi ya kufua umeme wa maji Rufiji MW2,115,kuboresha shirika la ndege Tanzania,ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge,kuendelea na utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara na uwekezaji.

“Aidha mpango wa maendeleo ya taifa 2019/20 umeweka msukumo katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza ikiwemo kupitia upya mfumo wa kitaasisi ,kisera na kisheria pamoja na kanuni zake ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi katika kuwekeza miradi ya maendeleo,” amesistiza.

Pamoja na mambo mengine alitaja kipaumbele cha kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mpango.

Pia amesema, miradi inayoendelezwa katika eneo hilo inalenga kuimarisha mfumo na taasisi za utekelezaji wa mpango,kuweka mfumo utakaowezesha upatikanaji wa uhakika wa rasilimali fedha na kuweka vigezo vya upimaji wa mafanikio kiutekelezaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!