Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bajeti 2019/20: Mawigi kutozwa kodi
Habari za Siasa

Bajeti 2019/20: Mawigi kutozwa kodi

Nywele bandia (mawigi)
Spread the love

BAJETI kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 iliyosomwa leo tarehe 13 Juni 2019, imependekeza ushuru kwa mawigi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 jijini Dodoma, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango amesema, mawigi yanayotengeneza ndani ya nchi, yatalipiwa ushuru wa asilimia Sh. 10,000 na yale kutoka nje ya nchi yatalipiwa asilimia Sh. 25,000.

Amesema kuwa, lengo la kuweka ushuru kwenye bidhaa hiyo inayopendwa na kutumiwa kwa wingi na wanawake nchini, ni kuongeza mapato kwa serikali.

Pendekezo hilo lilizaa shangwe bungeni huku baadhi ya wabunge wakichomekea bidhaa ya kucha bandia kwamba nazo zitozwe kodi.

Shangwe hilo liliibuka mara baada Dk. Mpango kupendekeza utozaji ushuru wa bidhaa hiyo ya nywele bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi.

“Napendekeza kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele bandia zinazotengemezwa ndani ya nchi, na 25 kwenye nywele bandia zinazoagizwa kutoka nje ya nchi lengo la hatua hizo ni kuongeza mapato ya serikali,” amesema Dk. Mpango.

Akichomelea katika mjadala huo huku sauti zikisika kutoka kwa baadhi ya wabunge wakitaja kucha bandia, Spika Job Ndugai amesema bado kucha bandia.

“Hapo inabidi wabunge iongezeke hiyo kodi eeh, waziri unaungwa mkono. Bado kucha bandia tumpe nafasi waziri,” amesema Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape awaomba wadau wa habari wamuamini

Spread the loveWAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

error: Content is protected !!