April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti 2019/20: Ada leseni za udereva, usajili magari wapanda

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania imependekeza kupanda kwa ada ya leseni ya udereva kutoka Sh. 40,000 za sasa, mpaka Sh. 70,000 kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 unaoanzia Julai Mosi mwaka huu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akisoma Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 leo tarehe 13 Juni 2019 bungeni jijini Dodoma, Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango amesema, kupandisha ada huku kunakwenda sambamba na kuongeza uhai wa leseni hizo kutoka miaka mitatu mpaka mitano.

Pia Dk. Mpango ameeleza kuwa, serikali imependekeza kuongeza tozo za usajili wa magari kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 50,000, kwa pikipiki za matairi matatu (bajaji) kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 30,000 na pikipiki za kawaida kutoka Sh. 10,000 hadi Sh. 20,000.

Akieleza sababu za kuongeza muda wa utoaji leseni pamoja na kuongeza ada hiyo Dk. Mpango amesema, lengo ni kupunguza gharama za kuchapisha leseni mara kwa mara kwa kuwa, leseni hizo zinaweza kudumu hata zaidi ya miaka mitano.

error: Content is protected !!