July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bajeti 2015/16 yapita kwa kishindo

Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya akiingia bungeni kusoma bajeti ya Serikali ya mwaka 2015/16

Spread the love

BAJETI ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/16 imepita kwa zaidi ya asilimia 80, hata hivyo malalamiko ya wabunge wameendelea kutawala. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Sehemu kubwa ya malalamiko kwa baadhi ya wabunge yaliitaka serikali kuangalia upya uamuzi wa kungeza kodi kwenye Mafuta ya Taa, Dizeli pamoja na Petroli.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alisema kuwa, ni lazima wananchi watoe fedha hiyo ili kurahisisha huduma ya umeme kusambaa vijijini.

Akizungumzia lalalamiko ya wabunge kuhusu ongezeko la tozo ya Mafuta ya Taa, Petrol na Dizel amesema, hakuna jinsi ya kukwepa tozo hiyo.

“Hatuwezi kuikwepa tozo hiyo kwani tunahitaji Sh.100 kwa kila lita moja na fedha hiyo ikikusanywa zinaweza kupatikana Sh. bilioni 276 kutokana na tozo ya mafuta kwa kila lita.

“Katika fedha hizo biloni 90 zitaelekezwa katika mfuko wa maji vijiji ili kuweza kuwapatia wananchi wa vijiji huduma hiyo ya maji kwa urahisi,” amesema Mkuya.

Amesema, hakuna njia yoyote wala miujiza yoyote ya taifa kuwa na maendeleo kama haitakuwa tayari kutumia kodi zake katika kufanya shughuli za maendeleo.

“Ni lazima wananchi wakachangia fedha hiyo ya Sh.100 na fedha hiyo tunaihitaji sana, hakuna njia ya kuweza kukwepo na lazima inapotokea changamoto yoyote wakati mwingine ichukuliwe kama fursa kwa sasa matumizi ya mafuta ya taa yamepungua.

“Lakini tukiweza kusambaza umeme wa kutosha jiijini hiyo ijulikane kuwa ni biashara kwani siyo kwa ajili ya kuwasha taa tu, bali ni kuweza kuutumia umeme huo kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji,” amesema Mkuya.

Hata hivyo, baada ya wabunge kupiga kelele kwa kuitaka serikali iongeza pensheni kwa wazee wastaafu, sasa serikali imekubali kuongeza pensheni kutoka Sh. 85,000 iliyokuwa imependekezwa na kufika Sh. 100,000.

Waziri Mkuya alitoa kauli hiyo alipokuwa akihitimisha mjadala wa siku saba wa kujadili Bajeti Kuu ya Mwaka wa Fedha 2015/16.

Na kwamba, serikali imekubali kuwalipa pensheni wazee wote nchini bila kujali kama walikuwa watumishi wa serikali.

Mkuya amesema, serikali imetenga fedha kwa ajili ya maofisa na watafanya uhakiki wa wazee hao ili kuweka miundombinu rafiki ambayo itawawezesha kulipwa fedha hizo.

Utaratibu ukikamilika amesema, wazee hao watatakiwa kulipwa kiasi cha Sh. 10,000 kwa mwezi ambapo kwa idadi ya sasa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ni wazee milioni 1.2 ambao watalipwa Sh.10,000 sawa na Sh. Bilioni 140 kwa mwezi.

Akiendelea kujibu hoja za wabunge wengi walilalamikia kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha za umma amesema, mpaka sasa wamebaini kuwepo kwa upotevu wa Sh. Bilioni 6 ambazo watumishi wa serikali kwa kushirikiana na wafanyakazi wa mabenki zimekuwa zikilipwa kama mafao ya wastaafu.

Akizungumzia kuhusu masuala ya uchumi amesema, ni kweli uchumi unaonekana kupanda lakini hali halisi ya Watanzania bado hawajaweza kuona uhalisi wa uchumi huo.

Akizungumzia kigezo cha serikali kukua kwa uchumi ni katika upatikanaji wa huduma za jamii kwa ujumla wake.

Amesema, kwa miaka mitano mfulilizo umasikini umepungua kwa asilimia 6.2 jambo ambalo linaonesha kuwa, zipo juhudi za makusudi za kupambana na umasikini.

Kuhusu matumizi ya Dola za Marekani Mkuya amesema, serikali bado inahitaji kuwa na dola za kutosha ambazo zitakuwa zimethibitiwa.

Amesema, kwa sasa Watanzania wanaishi kwa dola 1060 kwa mwaka na kuna upungufu wa dola 30 ili kufikia uchumi wa kati.

error: Content is protected !!