January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bahi: CCM imetufikisha hapa tulipo

Spread the love

WANANCHI wa Wilaya ya Bahi, Dodoma wamesema serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imekuwa chanzo kikubwa cha kuwasababishia umasikini wananchi hao. Anaandika Dany Tibason, Bahi … (endelea).

Mbali na hilo wamesema pamoja na kuwepo kwa rasilimali nyingi katika wilaya hiyo bado watendaji wamegeuka kuwa mwiba kwa wananchi kwa kuwatoza michango mingi isiyokuwa na taarifa ya mapata na matumizi.

Kwa upande wake aliyekuwa, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye ambaye pia amejiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) amesema mwaka huu ni mwaka wa kuizika serikali ya CCM na kuwashughulikia wezi wa mali za Umma.

Mbali na kutangaza kuizika CCM amewataka watanzania kupuuza vitisho ambavyo vinatolewa na wana CCM kwa madai kwamba upinzani ukichukua nchi kutatokea machafuko.

Sumaye alitoa kauli hiyo wilayani Bahi wakati wa mkutano mkubwa wa kuzindua kampeni ya ubunge uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi ya Bahi Sokoni wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa kumnadi mgombea ubunge Mathius Lyamunda (Chadema) ambaye anachuana na mtetezi wa jimbo hilo Omary Badweli (CCM).

Sumaye amesema kutokana na mfumo mbovu wa serikali ya CCM ndiyo maana kuna mfumko mkubwa wa bei za bidhaa na vyakula.

“Serikali imekuwa ikilalamika eti kuna mawaziri mizigo wanateuliwa na nani? Si kwa sababu ya kuteuliwa kishemeji shemeji kwa sasa serikali ya CCM ni sawa na shetani siyo CCM ya zamani,” amesema Sumaye.

Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Jimbo la Bahi kwa tiketi ya Chadema, Mathius Lyamunda amemuomba Mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA, Edward Lowassa kama akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kuhakikisha madini ya Uranium hayatoki wilayani Bahi.

Kauli hiyo ameitoa katika kiwanja cha Shule ya Msingi Bahi Sokoni katika mkutano wa kumnadi Mgombea huyo mara baada ya Lowassa kumtaka kuzitaja kero zinawahusu wananchi wa Jimbo la Bahi.

Lyamunda alimtaka Lowassa mara atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha madini ya Uranium hayatoki katika wilaya hiyo.

 

“Ndugu Rais watu wananchi wa Jimbo la Bahi kilio chao kikubwa wanataka usitishe mpango wa madini ya Uranium kutoka katika Jimbo hili,’’ amesema Lyamunda huku akishangiliwa.

Aidha Lyamunda pia amesema kilio kingine cha wakazi wa wilaya hiyo ni ukosefu wa maji kwa kuhakikisha yanapatikana ili kuondoa tatizo hilo ambalo limedumu kwa muda.

Amesema pia aliitaka serikali hiyo kusimamia suala la mradi Farkwa kwani utawafanya washindwe kufanya shughuli zao muhimu kama za ufugaji pamoja na umwagiliaji.

Lyamunda amesema suala la wafugaji kulipishwa michango mingi nalo limekuwa ni tatizo hivyo kama akipata nafasi aliangalie kwa umakini ili kuisaidia jamii ya Bahi kujikwamua kihuchumi na kuondokana na umaskini.

Kuhusu suhala la tatizo la maji Lyamunda amesema serikali inatakiwa kusitisha mara moja suala la kuziba mto Farkwa ambao unatililisha maji katika maeneo ya Bahi.

Amesema iwapo mpango wa serikali wa kuziba maji na kuruhusu asilimia kumi kama inavyokusudiwa ni wazi kwamba maendeleo katika wilaya ya bahi yatayumba.

“Maji yote ya farkwa lazima yaendelee kutililika na yasizuiliwe hivyo tunaomba mkakati wa kuziba maji usitishwe mara moja,” amesema Lyamunda na kuongeza:

“Mheshimiwa Rais pia kuna hili suala la Mto Bubu hasa huu mradi wa Farkwa maji kwenda Dodoma na asilima 10 kuja huku kwetu,hapa tunategemea kilimo na ufugaji, tunakuomba suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili wananchi waweze kutumia maji ya uhakika katika shughuli zao za maendeleo.”

“Maji ni jambo muhimu kwa maendeleo ya wananchi hivyo Mheshimiwa Lowassa tuna imani kubwa kwamba wewe ndiye rais hivyo jambo hilo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi mara tu uingiapo Ikulu ili kuwafanya wananchi kupata maji safi na salama pamoja na kuinua kipato kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji.”

Naye mgombea Urais kupitia (UKAWA) Edward Lowassa aliwahakikishia wakazi wa Jimbo hilo kama wakimpa nafasi kero zote walizonazo atahakikisha anazitatua.

Amesema ili kazi iweze kuwa nzuri na ya uhakika anawaomba wananchi wa Bahi na mikoa mbalimbali nchini kuhakikisha wanamchagulia wabunge wengi makini ambao wanatokana na Ukawa ili kuirahisisha kazi.

error: Content is protected !!