MBAHARIA mmoja wa Ukraine amekiri kujaribu kuizamisha boti inayomilikiwa na Mkuu wa kampuni ya silaha ya serikali ya Urusi, kwa lengo la kulipiza kisasi kwa uvamizi wa Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)
Boti hiyo yenye urefu wa mita 48 sawa na futi 157 inayoitwa Lady Anastasia, inayomilikiwa na Mkurugenzi mkuu wa Rosoboronexport, Alexander Mikheev ilikuwa imetia nanga huko Majorca nchini Hispania.
Baharia huyo mtaalamu wa ufundi alifungua ‘valves’ katika chumba chake cha injini kwa lengo la kuizamisha.
Alikamatwa na maofisa wa ulinzi wa raia siku ya Jumamosi tarehe 25 Februari, 2022 na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.
Alimwambia jaji wa mahakama moja nchini humo kuwa hajutii chochote na angeweza kufanya hivyo tena.
Mtu huyo alisema alijaribu kuizamisha boti hiyo ya Mikheev baada ya kutazama taarifa za habari kutoka Ukraine kwenye televisheni.
“Kulikuwa na video ya shambulio la helikopta katika jengo moja mjini Kyiv, walikuwa wakishambulia watu wasio na hatia,” alinukuliwa na vyombo vya habari nchini Hispania.
Siku ya Jumamosi, jengo la ghorofa ya juu karibu na uwanja wa ndege wa Zhuliany wa Kyiv nchini Ukraine lilipigwa kombora na kuacha shimo linalofunika angalau ghorofa tano.
Hakukuwa na maoni ya haraka kutoka kwa a Mikheev au kampuni ya Rosoboronexport, ambayo husafirisha bidhaa za ulinzi za Urusi, ikiwa ni pamoja na mizinga, magari ya kivita, ndege, meli, silaha na risasi.
Leave a comment