May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Babu Duni: Tukishirikiana tutaiondoa CCM 2025

Spread the love

MWENYEKITI wa chama cha ACT-Wazalendo Juma Duni Haji, amesema upinzani ukishirikiana uchaguzi ujao 2025 utaweza kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar…(endelea).

Duni ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 11 Mei 2022 akitoa salamu za chama chake katika kikao cha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“Tukisimama pamoja, tukitawanyika watatucheka na kwamba tulikuwa na Ukawa hapa vyama vinne tu tukaitoa CCM kutoka kushinda asilimia 86 mpaka 58,” amesema Duni.

Duni ambaye amewahi kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa Edward Lowasa kupitia Chadema mwaka 2015, amesema wakishindwa kushirikiana wataendelea kuwasindikiza CCM kubadilishana madaraka wenyewe kwa wenyewe.

“Tukishikamana 2025 tunawatoa, tukitengana tutaendelea kuwasindikiza wabadilishane sote tunahitaji mabadiliko la lazima mabadiliko yatokee.

“Kwanza lazima tupate Katiba Mpya na Tume Huru na kisha tupate uchaguzi ulio huru na wa haki 2025,” amesisitiza.

Amesema safari ya vyama vya upinzani ni moja nayo ni kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

“Tunahitaji mkitoka hapa tunakwenda kwa wananchi ili nyimbo iwe badala ya Salam Alekuum ukitazama hivi Katiba mpya, ukizunguka hivi katiba mpya ifike mpaka jikoni kule wanakopika kina mama kila mtu atamke katiba mpya,” amesema Duni.

Duni amesema chama chake kitashirikiana na Chadema kuhakikisha jambo hilo linasimama.

error: Content is protected !!