Tuesday , 16 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Babu Duni, Hamad wapitishwa kumrithi Maalim Seif – ACT Wazalendo
Habari za SiasaKitaifa

Babu Duni, Hamad wapitishwa kumrithi Maalim Seif – ACT Wazalendo

Spread the love

Halmshauri Kuu ya Chama imepokea na kuthibitisha mapendekezo ya Kamati Kuu ya Chama juu wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti wa Taifa na nafasi ya moja ya Mjumbe wa Halmshauri Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma leo tarehe 28 Januari, 2022 na Katibu wa Habari, Uenezi, na Mahusiano na Umma, Janeth Rithe imewataja waliopitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa ni Hamad Masoud Hamad na Juma Duni Haji.

 

Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na nguli wa siasa nchini, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alifariki Februari mwaka jana.

Aidha, aliyepitishwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa upande wa Zanzibar ni Othman Masoud Othman.

Othman ni Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Aidha, Halmashauri Kuu imekubali kujitoa kwa Juma Said Saanani katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Zanzibar.

Pia Halmashauri Kuu ya Chama imewapitisha wafuatao kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu wa Chama; Chrisant Joseph Msipi, Ester Thomas, Fidel Hemed Christopher, Fungo Godlove Benson, Jafet Mark Massawe, Johnson Mauma Gaugu na Msafiri Mtemelwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!