Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Babu Duni’ ajitosa kumrithi Maalim Seif -ACT- Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

‘Babu Duni’ ajitosa kumrithi Maalim Seif -ACT- Wazalendo

Juma Duni Haji
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazaendo – Zanzibar, Juma Duni Haji maarufu kama ‘Babu Duni’ amejiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho kwa lengo la kuwania nafasi ya uenyekiti Taifa ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya Halmashauri Kuu ya chama hicho, kutangaza nafasi hiyo kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa marehemu Maalim Seif Sharif Hamad aliyefariki tarehe 17 Februari 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 1 Novemba, 2021 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma ACT Wazalendo, Janeth Rithe, Duni amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Amesema katika barua hiyo ya tarehe 30 Oktoba 2021 Duni ameweka bayana kuwa amejiuzulu nafasi hiyo kwa sababu ana nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, hivyo amejiuzulu ili nafasi hizo mbili zitangazwe pamoja.

Rithe amesema katika kikao cha halmashauri hiyo kilichoketi jana tarehe 31 Oktoba 2021, mbali na kutangaza nafasi ya Mwenyekiti wa chama pia kilitoka na azimio la kutangaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, na nafasi moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu.

“Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar na uchaguzi wa nafasi moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ambayo nayo ipo wazi utafanyika kupitia Mkutano Mkuu wa Chama Taifa utakaofanyika tarehe 29 Januari 2021.

“Pili, Halmashauri Kuu ya Chama Taifa ilipokea Taarifa ya Kamati Kuu juu ya ufanisi wa Ngome za Chama za Wanawake, Vijana na Wazee.

“Kwenye taarifa hiyo ambayo Halmashauri Kuu iliiridhia, Ngome ya Vijana imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwasemea vijana wa Tanzania na Watanzania kwa ujumla mathalani kwenye suala la mikopo ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu,” amesema.

Aidha, amesema katika kuimarisha utendaji, Halmashauri Kuu ya Chama kwa kuzingatia Ibara ya 94(3)(iii) ya Katiba ya ACT Wazalendo, imemteua Sevelina Joseph Mola kuwa Naibu Katibu Bara wa Ngome ya Vijana Taifa.

Amesema kwa upande wa Ngome ya Wanawake, awali Kamati Kuu ya Chama Taifa, kwa mujibu wa madaraka yake chini ya Ibara ya 79(1)(x) imeuvunja uongozi wa kitaifa wa Ngome ya Wanawake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Badala yake, Kamati Kuu imeunda Kikosi Kazi cha Ngome ya Wanawake Taifa ambacho viongozi wake ni; Pavu Abdallah: Mwenyekiti, Bonifasia Mapunda: Katibu, Halima Ibrahim: Mjumbe, Annamerrystella Mallack: Mjumbe na Sevelina Mwijage: Mjumbe,” amesema.

Pia amesema Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imeazimia kwa kauli moja kuwa Chama kiendelee kwa kasi zaidi kuipigania Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

“Halmashauri Kuu imeazimia kuwa Chama kitakuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi ya kiuchaguzi ili chaguzi zijazo kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC) na zile za Zanzibar (chini ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC) ziwe huru, za haki na za kuaminika.

Kwa upande wa fedha za tozo na zile za Shirika la Fedha Duniani (IMF), amesema Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imewaagiza viongozi wa Majimbo yote nchini kuweka mfumo maalum wa kufanya ukaguzi wa umma wa fedha hizo katika maeneo yao.

Wakati kimataifa, amesema Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imepongeza mwenendo wa Chama kuendelea kusimama na makundi mbalimbali duniani yanayokandamizwa na kuonewa na imetoa maazimio mahsusi yafuatayo;-

Aidha, amesema Halmashauri hiyo ilipokea taarifa ya Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe kwa madaraka aliyonayo chini ya Ibara ya 83(1)(c) ya Katiba ya ACT Wazalendo kumteua Prof. Omar Fakih Hamad Mwakilishi wa Jimbo la Pandani na Mnadhimu wa Wawakilishi wa ACT Wazalendo kwenye Baraza la Wawakilishi kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!