May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baba mzazi wa DED Kiteto, Balozi Nchimbi afariki dunia

Spread the love

 

JOHN Alphoso Nchimbi, baba mzazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto (DED), Mkoa wa Manyara, John Nchimbi amefariki dunia, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mzee Nchimbi ambaye ni mwanasiasa mkongwe nchini na mwanachama wa Chama Cha mapinduzi (CCM), amefikwa na mauti usiku wa kumakia leo Jumapili, Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam.

John amesema, “kwa huzuni kubwa sana, Leo nimempoteza my mentor, my hero, my love, my protector my everything aliyenipenda sana, aliyenitunza na kunilea, baba yangu mzazi.”

Aidha, Mzee Nchimbi ni baba mzazi wa aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Balozi Emmanuel Nchimbi.

Msiba upo nyumbani kwa Mzee Nchimbi, Tabata Relini jijini Dar es Salaam ambapo taratibu za mazishi zinafanyika.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!