December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baba mbaroni kwa kumbaka na kumlawiti mwanae

Wilbroad Mutafungwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro

Spread the love

MWANAUME mmoja Saidi Kasti (35) mkazi wa kitongoji cha Kimangakene Kijiji cha Diyovuva kata ya  Kiroka wilayani Morogoro anashikiliwa polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto wake wa kike wa kumzaa mwenye umri wa miaka miwili. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Akizungumzia tukio hilo mama wa mtoto huyo, Himaya Waziri alisema tukio hilo lilitokea tarehe 7 Julai, 2019, majira ya saa 7 usiku baada ya baba huyo kwenda kulala na watoto wake katika chumba kingine kuanzia tarehe 6 Julai, licha ya yeye kumzuia ambapo alisikia mwanaye huyo aliyebakwa akilia na ndipo alipokwenda kumbembeleza na hatimaye alilazimika kumchukua na kwenda kulala nae.

Akielezea tukio hilo mama huyo alisema, baada ya yeye kujifungua mtoto wa tatu waliamua kulala vitanda tofauti kwenye chumba kimoja huku yeye akiwa na watoto wawili kitandani na yeye akiwa na mtoto mchanga ambapo Jumamosi ya tarehe 6 Julai, aliamua kwenda kulala na watoto katika chumba kingine ambacho alikuwa analala mtoto wake mkubwa aliyeondoka.

“Ilipofika usiku wa saa 7 alisikia sauti kali ya mtoto akilia huku yeye (baba) akisema nae, na alipoulizwa alidai mtoto amejinyea ndipo mama uyo alipoenda kumchukua sababu alikuwa analia sana na baadae akamuangalia vizuri akaona hayupo vizuri sehemu ya siri za nyuma,” alisema mama huyo.

Alisema, kulipokucha walichukua uamuzi wa kwenda kituo cha Afya Kiroka na ndipo ilipobainika kuwa mtoto huyo alikuwa amebakwa na kulawitiwa na kutakiwa kwenda hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro ambapo nao waligundua tatizo hilo na kuamua kumlaza mtoto huyo kwa ajili ya kuendelea na matibabu wodini.

Akizungumzia hali ya mtoto huyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro, Dk. Rita Lyamuya alisema, wamempokea mtoto huyo na kwamba amelazwa wodi namba 7B akiwa inasemekana amefanyiwa tendo la kubakwa na hospitali imempokea na inaendelea kufanyia uchunguzi huku hali yake ikiwa inaendelea vizuri.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro (SACP), Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kufuatia tukio hilo licha ya kwamba taarifa za awali zinadai kuwa mtuhumiwa alifanya kitendo hicho kutokana na imani za kishirikina ili aweze kupata utajiri kupitia shughuli zake mbalimbali anazofanya.

error: Content is protected !!