POLISI wa jimbo la Lagos nchini Nigeria wamemtia mbaroni mwanaume mmoja kwa madai ya kuyaondoa matiti ya binti yake mwenye umri wa miaka nane kwa kutumia jiwe la moto. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).
Baba huyo aliyefahamika kwa jina la Banjo Adegboyega anadaiwa kutekeleza unyama huo ili kuzuia chuchu za binti yake zilizokuwa zimeanza kukua kutokana na mabadiliko ya mwili.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Msemaji wa polisi wa jimbo hilo, DSP Asijebotu amesema wanamshikilia mwanaume huyo ambaye pia ni Mhandisi ili kurahisisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Amesema kwa sasa msichana huyo amelazwa hospitalini kwa matibabu, huku ripoti zikisema kuwa yuko mahtuti kutokana na majeraha aliyosababishiwa na baba yake mzazi.
Aidha, taarifa za Baba huyo kutekeleza ukatili huo ziliripotiwa polisi na Mtandao wa Kikundi cha wanaharakati wa kutetea haki za watoto.
Mkuu wa mtandao huo, Ebenezer Omejalile amewaeleza waandishi wa habari kuwa mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Panel, “aliyabana na kisha kuyachoma matiti ya binti yake.
“Baba wa msichana huyo alitumia jiwe la moto alilolifunga ndani ya nguo na kumchoma hadi alipohakikisha kuwa ameyaharibu kabisa matiti ya binti yake,” alisema.
Alisema pia kwamba baba huyo alielezea kutoridhishwa kwake na jinsi binti yake alivyokuwa ameanza kuonyesha dalili za saratani ya matiti kwenye matiti yake ndio maana alitaka kuyazuia yasiote.
“Jambo la kushangaza ni jinsi baba huyo alivyosema amekuwa akimuogesha binti yake wa miaka 8 kila siku,” amesema.
Mama yake msichana huyo alisema Banjo amekuwa akimpiga binti yake mara kwa mara.
Leave a comment