August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baba Kundambanda afariki Dunia

Spread the love

ISMAIL Issa Makombe ‘Baba Kundambanda’, msanii maarufu wa vichekesho na aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Masasi kwa tiketi ya CUF, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, anaandika Hamisi Mguta.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Baraka Sandale, rafiki wa karibu wa msanii huyo amesema marehemu amefariki kwa matatizo ya pumu ambayo alikuwa na matatizo kwa muda mrefu.

Sandale amesema, juzi marehemu alizidiwa na kufikishwa katika hospitali ya Mkomaindo na kupatiwa matibabu na kuruhusiwa, lakini hali ilikuwa mbaya usiku wa kuamkia leo.

“Hali ilizidi kua mbaya iliyopelekea marehemu kushindwa kupumua, hata hivyo hatukufanikiwa kumfikisha tena hospitali ndipo mauti yakamfika alfajiri,” amesema Sandale ambaye alipokea simu ya marehemu iliyopigwa na Mwandishi wa Mtandao huu.

Taarifa za awali kutoka kwa Sandale zinaeleza huenda mwili wa marehemu huyo ukazikwa kesho lakini taarifa kamili zitatolewa.

Kundambanda alitamba zaidi katika kipindi cha ‘Vituko Show’ akiigiza kwa rafudhi ya kimakonde, kabla ya kuingia katika siasa na kugombea ubunge jimbo la Masasi, Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

error: Content is protected !!