October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baba amuua bintiye, kisa kujiozesha

Romana Ashrafi, enzi za uhai wake

Spread the love

ROMANA Ashrafi (14), raia wa Iran, ameuawa kwa kushambuliwa kwa mundu na baba yake mzazi Reza Ashraf, kwasababu ‘alijiozesha.’ Nchini humo mauaji hayo yanaitwa ‘mauaji ya heshima.’ Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Kwa utamaduni wa Iran, ‘mauaji ya heshima’ ni mauaji ya ndugu wa familia ambaye anadaiwa kupeleka aibu miongoni mwa watu wa familia.

Taarifa zaidi nchini humo zinaeleza, binti huyo alitoroka nyumbani kwao na mpenzi wake, Bahamn Khavari (35) na kukimbilia mji wa Talesh baada ya baba yake kupinga wawili hao kufunga ndoa.

Siku tano baada ya Bahamn na Romana kutoroka, taarifa ziliwafikiwa polisi na kuanza kuwasaka wiki iliyopita.

Baada ya kupatikana kwao, Romana aliwaambia maofisa hao kwamba anahofia maisha yake pale ataporejesha kwa baba yake. Hata hivyo, ‘alipuuzwa.’

Baada ya kurejeshwa nyumbani, kwa hasira baba yake alimkakataka kwa mundu na kisha kukiri kufanya hivyo.

Tayari Reza anashikiliwa na vyombo vya usalama vya taifa hilo, mauaji hayo yameibua hisia kali nchini humo na kutuhumu sheria kushindwa kuwalinda wanawake.

Sheria za nchi hiyo zinawapunguzia adhabu wazazi wanaofanya mauaji kwa jina la ‘mauaji ya heshima’ na adhabu yake kuwa kati ya miaka mitatu hadi 10.

error: Content is protected !!