Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Baba aliyefiwa watoto, mke atoa yamoyoni
Habari MchanganyikoTangulizi

Baba aliyefiwa watoto, mke atoa yamoyoni

Spread the love

 

MAMIA ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya wanandugu watano, wanaodaiwa kufariki dunia katika shughuli ya kuagwa kwa mwili wa Dk. John Pombe Magufuli. Anaripoti Yusuf Katimba…(endelea).

Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya tarehe 21 Machi 2021, katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo maelfu ya wakazi wa mkoa huo na maeneo jirani, walijitokeza kuuaga mwili wa Dk. Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania.

Miongoni mwa waliohudhulia kwenye kuaga miili ya ndugu hao leo Alhamisi tarehe 25 Machi 2021, ni Mbunge wa Kibamba (CCM), Issa Mtemvu.

Waliofariki dunia ni, Susan Mtuwa na watoto wake wawili, Natalia (5) na Nathan (6) pamoja na watoto wengine wawili wa shemeji yake, Susan ambao ni Michelle Harry Mtuwa (8) na Christian Allan Mtuwa (11).

Kutokana na vifo hivyo, Denis Mtuwa ambaye ni mme wa Susan na watoto wawili, ametoa lawama zake kwa Serikali.

Akizungumza na MwanaHALISI Online nyumbani kwake mahali shughuli za msiba huo zikiendelea amesema, kuvurugwa kwa ratiba ya kuanza shughuli ya kumuaga Rais Magufuli, kunaweza kuchangia sababu za vifo vya mke na watoto wake.

“Tulikubaliana na mke wangu waende mpema na kisha warudi ili twende kanusani.”

 

“Tulifanya hivyo kwa sababu niliamini iwapo kuaga mwili wa Rais Magufuli ingeanza saa mbili kama ilivyotangazwa, wangewahi kutoka na kurudi ili twende kanIsani, lakini ratiba haikua hivyo,” amesema.

Akizungumza huu akitokwa kwikwi, Denis amesema, yeye na mkewe Susan Ndana Mtuwa walikuwa na ratiba nyingine, lakini walishindwa kutoka uwanjani kabla ya watu kuongezeka kwa kuwa walikuwa hawajamuaga Rais Magufuli.

Majeneza matano ya miili ya wana ndugu hao, yalifikishwa nyumbani kwao Kimara jana jioni na kulazwa hadi leo ambapo baadhi ya ndugu, wameaga miili ya wapendwa wao kisha kupelekwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kimara.

 

Kanisa hilo, ndilo ambalo Denis Mtuwa na mkewe Susan, walifunga ndoa miaka kumi iliyopita.

Awali, akizungumza nyumbani hapo, Mbunge Mtemvu amesema, alikuwa Dodoma akielekea Chato mkoani Geita katika mazishi ya Hayati Magufuli yanayofanyika kesho Ijumaa, “lakini kutokana na msiba huu nimelazimika kurejea kuwapa pole wenzangu.”

Baada ya mwili wa wanafamilia hao kuagwa nyumbani kwao, umepelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ambapo miili hiyo inatarajiwa kuzikwa saa nane mchana wa leo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!