Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Baada ya siku 342 gerezani, DPP awafutia mashtaka bosi MSD, mwenzake
Habari MchanganyikoTangulizi

Baada ya siku 342 gerezani, DPP awafutia mashtaka bosi MSD, mwenzake

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wawili hao, wameachia huru leo Alhamisi, tarehe 13 Mei 2021, na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele.

Ni baada ya wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kuwasilisha hati ya kuwafutia mashtaka washtakiwa hao, iliyosainiwa na aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga tarehe 10 Mei, 2021, akionesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.

          Soma zaidi:-

Hadi wanaachiwa huru, wawili hao, wamekaa gerezani kwa siku 342 kuanzia tarehe 5 Juni 2020, walipofikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, wakitokea Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo utakatishaji fedha haramu zaidi ya Sh.1.6 bilioni.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa kati ya tarehe 1 Julai, 2016 na 30 Juni 2019, maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.

Pia, washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia MSD hasara ya Sh.3.8 bilioni

Inadaiwa Bwanakunu akiwa ni mtumishi wa umma alifanya matumizi mabaya ya madaraka kwa kongeza mishahara na posho za wafanyakazi bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi na kuisababishia MSD hasara ya Sh Sh.85.1 milioni

Katika shtaka jingine, ilidaiwa kati ya tarehe 1 Julai 2016 na 30 June 2019, katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar wa Salaam wote kwa pamoja walijipatia fedha Sh 1.6 bilioni wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu ambao ni kuongoza genge la uhalifu.

Ni baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.

Biswalo kwa sasa ni Jaji wa Mahakama kuu ambaye aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Tarehe 11 Mei 2021, anasubili kaupishwa yeye pamoja na wenzake 28

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

error: Content is protected !!