Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Baada ya Segerea, Mbowe kuongoza Kamati Kuu leo
Habari za SiasaTangulizi

Baada ya Segerea, Mbowe kuongoza Kamati Kuu leo

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa, pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu wanakutana leo tarehe 30 Machi 2019 kujali hali ya kisiasa nchini. Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza kuwa, kikao hicho ni cha siku moja na kilichofanywa kwa mujibu wa Katiba ya Chadema toleo la mwaka 2016.

Kikao hicho kitaongozwa na Mbowe, ikiwa ni baada ya kukosa vikao kadhaa kutokana na kuwekwa rumande katika Gereza la Segerea tangu Novemba mwaka jana mpaka alipopata dhamana tarehe 7 Machi 2019.

Kazi zinazotarajiwa kufanywa na kamati hiyo ni pamoja na kupokea taarifa na kujadili mwenendo wa kisiasa nchini, na kisha kuchukua mwelekeo baada ya mjadala wa taarifa hiyo.

Kamati Kuu hiyo inakutana ikuwa ni baada ya siku nne viongozi wakuu wa vyama vya upinzani nchini, kukutana na kujadili mwenendo wa hali ya siasa nchini.

Mkutano viongozi hao wakuu uliitishwa baada ya Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano wa Chama cha ACT-Wazalendo kwa madai kwamba, Chama cha Wananchi (CUF) kilipanga kufanya vurugu. Mkutano wa viongozi hao ulidumu kwa saa tatu.

Viongozi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni jijini Dar es Salaam ni pamoja na Mbowe; Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim; Kiongozi wa ACT,  Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Yeremia Maganja pamoja na mwanachama mpya wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Shariff Hamad.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!