Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Baada ya mahabusu; Mbowe akutana na janga jingine
Habari za SiasaTangulizi

Baada ya mahabusu; Mbowe akutana na janga jingine

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, anakumbana na misukosuko mfululizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Uongozi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro umekusudia kupoka kiwanja cha Mbowe ambacho kimeingizwa kwenye orodha ya viwanja 34 vinavyokusudiwa kutwaliwa na serikali.

Kwa muzibu wa taarifa kutoka Hai ni kuwa, tayari Willium Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameandikiwa ilani ya ubatilisho wa kiwanja viwanja hivyo.

Lengai Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai amedai kuwa, hatua hiyo inatokana na Mbowe pia wamiliki wengine wa viwanja hivyo kushindwa kulipa kodi ya pango la ardhi.

Hata hivyo Mbowe ameuambia mtandao huu kwamba hajapata taarifa hiyo vizuri na kwamba, anafuatilia. “Bado sijajua vizuri mpaka nifuatilie,” amesema.

Majina mengine yaliyoorodheshwa na Ole Sabaya kwa madai ya kushindwa kulipa jumla ya Sh. 1,828,166,096 ni Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd; Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Cynthia Ngoye; wafanyabiashara wanaomiliki shule binafsi na kampuni za utalii.

Ole Sabaya alifikia uamuzi huo jana tarehe 13 Machi 2019 baada ya kufanya ziara ya kusikiliza malalamiko na migogoro ya ardhi wilayani Hai.

Kwenye mkutano huo Ole Sabaya amelalamika kuwa, watu wamepewa viwanja muda mrefu lakini wameshindwa kuviendelea kwa kujenga viwanda.

Jacob Muhumba, Ofisa Ardhi Wilaya ya Hai kwenye mkutano huo alimwambia Ole Sabaya kuwa, watu wengi waliopewa viwanja, walipewa tangu mwaka 1984, 2001 na 2004 pamoja na hivyo wengi hawajaviendeleza.

Tarehe 13 Juni 2017 Serikali ya Hai  iliondoa miundombinu ya uzalishaji katika shamba la Kilimanjaro Veggies linalomikiwa Mbowe  kwa madai kuwa, lilikuwa ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.

Pamoja na kuondoa miundombinu hiyo, Serikali ilimtaka Mbowe kulipa Sh 18 Milioni 18 kutokana na uharibifu wa mazingira aliofanya kwenye chanzo hizo. Pia alitakiwa kulipa gharama zote zilizotumika kuondoa miundombinu kwenye shamba hilo.

Baadaye Mahakama Kuu Moshi (Moshi Registry)iliruhusu shughuli za kilimo kuendelea kwenye shamba hilo huku kesi ya msingi ikisubiriwa kusikilizwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!