September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Baada ya kukataa chanjo kwa miezi 6… Rais DRC achanja

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi akichanjwa chanjo ya Corona

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi mapema wiki hiii amepokea dozi yake ya kwanza ya chanjo dhidi ya Covid-19. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hatua hiyo imekuja ikiwa imepita miezi sita tangu alipokataa kuchanja chanjo aina ya Astra Zeneca na kuibua mjadala dhidi ya wakosoaji wake nchini humo.

Licha ya kwamba ofisi ya rais haikutaja aina ya chanjo ambayo Rais Tshisekedi alikuwa amedungwa, chanjo za Moderna na AstraZeneca ndizo zilizosambazwa nchini humo.

Mkuu wa huyo wa nchi, ambaye alikuwa ameambata na mkewe Denise Nyakeru, alisema, “chanjo ni suluhisho bora zaidi ya kupambana na Covid-19 kwa sasa. Kwa kuwa nimepoteza ndugu kadhaa kwa ugonjwa huo, niko katika nafasi nzuri ya kutoa ushahidi kuhusu athari mbaya za janga hili. ”

Rais Tshisekedi alisema wakongomani wanapaswa kufanya kila juhudi kupata chanjo.

Wakati juhudi za kampeni za kuhamasisha watu zaidi waendelee kuchanja, Wakongo wengi wanaonyesha kutoridhishwa kwao na chanjo hizo.

Wizara ya Afya nchini humo imeonyesha kuwa kuenea kwa Covid-19 kumepungua katika mji mkuu Kinshasa, ambao hapo awali ulikuwa ndio kitovu kusambaa kwa ugonjwa huo nchini DR Congo.

Tangu kesi ya kwanza iripotiwe nchini humo, jumla ya watu 54,009 wameambukizwa kati yao 1,061 wamefariki duniani kutokana na Covid-19.

Aidha, Waziri wa Afya ya Umma Jean-Jacques Mbungani alitangaza kuwa nchi hiyo itapokea chanjo za Johnson na Johnson na Pfizer.

error: Content is protected !!