Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Baada ya kuhukumiwa kulipa mamilioni, Mbowe na wenzake walala Segerea
Habari za SiasaTangulizi

Baada ya kuhukumiwa kulipa mamilioni, Mbowe na wenzake walala Segerea

Spread the love

VIONGOZI wanane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chademawakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, wamenusurika kufungwa gerezanibaada ya kuamriwa kulipa faini ya fedhataslimu zaidi ya Sh. 350 milioni kwakukutwa na hatia ya makosa ya uchocheziAnaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Makosa hayo ni yale yaliyotokana namaandamano waliyoyafanya tarehe 16 Februari 2018 wakitoka kwenye mkutanowa kampeni ya uchaguzi mdogo wa ubungejimbo la Kinondoni, kwenda ofisi zaMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yaWilaya, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mbowe, wengine ni John Mnyika(sasa Katibu Mkuu), Halima Mdee(Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Bawacha), Esther Matiko (Mwenyekiti waKanda ya Serengeti), Salum Mwalimu(Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), John Heche(Mbunge wa Tarime) na Ester Bulaya(Mbunge wa Bunda mjini).

Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ametoa hukumu katika mashtaka 12 kati ya13, yaliyokuwa yanawakabili viongozi hao, shitaka moja likiwa limeondolewa, baada yaupande wa mashtaka kushindwakulithibitisha.

Dk. Vincent Mashinji, aliyekuwa KatibuMkuu wa chama hicho na ambaye alihamana kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivi karibuni, naye amekutwa na hatia nakuamriwa kulipa faini vilevile kutokana nakesi Na. 112/2018 iliyowahusu.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Mbowe pekeyake anaongoza kwa kiwango cha fainiakiwa ameamriwa kulipa faini ya jumla yaSh. milioni 70.

Hakimu Simba amesema washtakiwa wotehao wamehukumiwa kwa pamoja katikamashtaka manne, wakati mashtakayaliyobaki yakihukumiwa kwa kila mmojana makosa yake.

Amesema washtakiwa hao wamepigwa fainiya Sh. milioni 10 au kifungo cha miezimitano gerezani kwa kila shtaka, katikamashtaka matatu, na Sh. milioni 5 katikashtaka la tisa.

Mashtaka hayo manne ni shtaka la pili la kufanya mkusanyiko kinyume na sheria, la tatu kufanya mkusanyiko wenye vurugu, la tisa ni uchochezi wenye lengo la uasi,wakati shtaka la mwisho likiwa la nne nikukaidi amri ya polisi ya kuacha kufanyamkusanyiko usio halali.

Mahakama hiyo pia imetoa hukumu ya fainiya Sh. milioni 10 au kifungo cha miezimitano gerezani kwa Mbowe, Msigwa, Mdee, Heche na Bulaya kwa kila kosa katikamashtaka matatu.

Mashtaka hayo matatu ambayo Mboweamekutwa na hatia peke yake ni shtaka la tano na la sita ya kuchochea chuki, nashtaka la 11 la kuchochea watu kufanyamakosa.

Mbowe pia amehukumiwa kulipa faini yaSh. milioni 5 au kifungo cha miezimitano gerezani katika shtaka la 10.

Kutokana na hukumu hiyo, Mboweamekutwa na hatia katika mashitakamanane na kuhukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni 60 kwa mashtaka sita na Sh. milioni10 kwa mashtaka mawili (jumla Sh. milioni70) au kwenda jela miezi 40.

Katika shtaka la 12, Mchungaji Msigwa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa, amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni 10 au kifungo cha miezi mitano gerezani baadaya kukutwa na hatia katika mashtakamatano. Anatakiwa kulipa Sh. milioni 45 au kutumikia kifungo cha miezi 25 gerezani.

Mdee ambaye amekutwa na hatia katikamashtaka matano, likiwemo la saba la kuleta chuki, amehukumiwa kulipa faini yaSh. milioni 10 au kifungo cha miezi mitanojela. Kwa hivyo, anatakiwa kulipa faini yaSh. milioni 45 au kwenda jela miezi 25.

Heche ambaye naye amekutwa na hatia nawenzake katika mashitaka matano, amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni 10 au kwenda jela miezi mitano; akihusishwana shtaka la nane la kufanya uchocheziwenye kuleta chuki kwa jamii.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, Hecheanatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 45 au kwenda jela miezi 25 hukumu ya hatia yamashitaka matano.

Bulaya amehukumiwa kulipa faini Sh. milioni 10 au kifungo cha miezi mitanogerezani baada ya kukutwa na hatia kwashtaka la 13 la kushawishi watukuandamana.

Bulaya amekutwa na hatia katika mashtakamatano na kwa pamoja anatakiwa kulipafaini ya Sh. milioni 45 au kwenda jela miezi25.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!