August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baada ya kufuta ada, Serikali kupitia miongozo kupunguza michango shuleni

Wanafunzi wakishangilia baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inajipanga kupitia upya miongozo ya kujiunga shule za sekondari na kidato cha tano na sita, ili kupunguza masuala yanayoongeza michango ya wanafunzi shuleni isiyo na tija. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, tarehe 24 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolph Mkenda, akijibu hoja zilizoibuliwa na baadhi ya wabunge katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali, kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Katika majadala huo, baadhi ya wabunge waliiomba Serikali itatue changamoto ya utitiri wa michango ya wanafunzi shuleni, ili azma yake ya kufuta ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha tano na sita kwa ajili ya kuwapunguzia mzigo wananchi, iwe na tija.

“Hii sehemu ya gharama ya kusoma, tutapitia miongozo yote. Tutashirikiana na Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Hazina, kuangalia miongozo ili kusiwe na mzigo mkubwa ambao unakinzana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan, ya kutoa elimu bila ada,” amesema Prof. Mkenda.

Prof. Mkenda amesema “tutafanya haraka kupitia Join Instructions (fomu za kujiunga) zote na kuangalia mizigo ipi imewekwa ambayo wabunge wamesema tumeondoa Sh. 70,000 ya ada, lakini gharama nyingi ziko sehemu nyingine. Tutafanya kazi kuhakikisha tunapunguza michango yote ambayo haina maana na tija.”

Aidha, Prof. Mkenda amesema, katika bajeti ya 2022/23, Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), imetenga fedha kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wanaotika katika kaya masikini.

error: Content is protected !!