Monday , 22 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Baada ya Jerusalem Trump ataka Irsael itwae mlima Golan, Syria
Kimataifa

Baada ya Jerusalem Trump ataka Irsael itwae mlima Golan, Syria

Spread the love

BAADA ya kuteka Mji wa Jerusalem kutoka Taifa la Palestina na kuukabidhi kwa Israel, sasa Donald Trump, Rais wa Marekani anaelekeza nguvu kuuteka mlima wa Golan, Syria kwa dhamira ile ile ya kuukabidhi kwa Utawala wa Israel. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Trump Trump ameonesha nia ya kubadilisha Sera ya Marekani ya kutambua mlima wa Golan kuwa mali halali ya taifa la Syria ambapo ameweka pendekezo ili taifa lake litambue kuwa ni mali ya Israel.

Hata hivyo, msimamo huo wa Rais Trump umepingwa vikali na Rais wa Baraza la Uhusiano wa Kigeni Marekani  ambaye pia ni Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Kigeni, Richard Haass.

Hatua hiyo ya Trump inapingana vikali na msimamo wa mtangulizi wake, Barrack Obama aliyepinga Israel kuwa mmiliki wa milima golani. Kwa kupiga kura ya kuunga mkono azimio la baraza la usalama wa umoja wa mataifa.

Mwaka 1981 bunge la Israel lilipitisha sheria ya usimamizi na umiliki wa milima ya golani, hatua hiyo iliibua Umoja wa Mataifa, ambapo kupitia baraza lake la usalama ililaani hatua hiyo likisema ni haramu.

Hadi sasa kuna raia takribani 20,000 walioanzisha makazi 30 kwenye milima ya golani. Lakini Sheria ya Kimataifa inayatambua makazi hayo kuwa ni haramu.

Israel iliteka eneo hilo mwishoni mwa vita ya mashariki ya kati na kuzuia jaribio la Syria la kulikomboa eneo hilo wakati wa vita vya 1973.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!