July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Baa la njaa Mpwapwa, wananchi wala pumba

Spread the love

WAKAZI wa mkoa wa ¬†Dodoma hususani wilaya ya Mpwapwa wanakabiliwa na njaa hadi kufikia hatua ya wakazi hao kula pumba, ubuyu na matunda ya porini huku serikali ikichelewa kupeleka chakula cha msaada. Anaandika Dany Tobason, Mpwapwa … (endelea).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa jana, wakazi hao, wamesema wamefikia hatua hiyo ya kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu tatizo hilo baada ya kuona viongozi wa Mkoa huo kukaa kimya.

Wamesema kutokana uhaba huo wa chakula unaowakabili kwa zaidi ya miezi mitatu, wanaomba serikali kuhakikisha kufikisha chakula cha msaada kama ilivyowaahidi.

“Hivi sasa tunashindwa hata kuendesha shughuli zetu za kilimo na baadala yake tumekuwa manamba kwa kufanya kazi kwa matajiri ili kupata ujira mdogo ili tuweze kujikimu, amesema mmoja wa wakazi hao huku akiungwa mkono na wenzake aliyofuatanao.

Wamesema kama serikali haitakuwa makini, kuna uwezekano mkubwa kwa wilaya hiyo ikaja kuendelea kukabiliwa na njaa kwa muda mrefu kutokana na wakazi hao kushindwa kuendesha kilimo katika mashamba yao wakati huu wa msimu na baadala yake kwenda kufanya kazi za vibarua vya kulima mashamba kwa matajiri.

Wakazi hao wamesema suala hilo la uhaba wa chakula katika wilaya hiyo linafahamika kuanzia viongozi wa wilani hadi mkoa, kwamba lilianza tangu kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu ambao umemuingiza madarakani Rais John Magufuli.

Aidha, Wakazi hao wamesema hali hiyo imefikia hapo baada ya viongozi wa wilaya na mkoa kuona aibu kulizungumzia waziwazi suala hilo, wakati wananchi wanaendelea kuathirika.

“Msaada wa chakula unaohitajika ni zaidi ya tani 15, 000, ambazo zikipatikana zitasaidia na kutufanya tutulie na kutuwezesha kulima mashamba yetu,” amesikika akisema mmoja wa wakazi hao.

Alipotafutwa Mbunge wa Jimbo hilo, George Lubeleje, ili kulitolea ufafanuzi tatizo hilo, hata hivyo, alishindwa kufanya hivyo kwa vile wakati huo alikuwa katika msiba wa mmoja wa mwanachama mwenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hivi karibu Mkuu wa Mkoa huo, Chiku Galawa, akiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani wilayani hapa alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa tatizo hilo linafahamika lakini kulikuwa na ukosefu wa taarifa sahihi kuhusu tani za chakula hicho cha msaada kinachohitajika.

Alisema taarifa hiyo ilionesha kuwa msaada unaotakiwa katika wilaya hiyo kuwa sawa na chakula chote kinacholimwa mkoani humo, jambo alilolitilia shaka.

error: Content is protected !!