January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azzan, Mkullo, Misanga “wachemsha”

Mbunge wa CCM Wilaya ya Kilosa, Mstaafa Mkulo

Spread the love

UTAFITI wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo na Kuondoa Umaskini (Repoa) umebaini kuwa majimbo matatu ya ya Kinondoni, Singida Magharibi na Kilosa, yametumia vibaya fedha za mfuko wa jimbo (CDF). Anaandika Sarafina Lidwino…(endelea)

Katika utafiti  wao wa masuala ya utawala bora na maendeleo, uliowasilishwa leo, majimbo hayo ni kati ya sita yaliyofanyiwa utafiti na Repoa kwa kushirikiana na wadau kutoka Policy Forum.

Pia, majimbo mengine ya Karatu, Siha na Lindi Mjini yamebainika kutumia fedha hizo vizuri kama ilivyopangwa.

Wabunge wa majimbo hayo ni Idd Azzan (Kinondoni), Mohamed Misanga (Singida Magharibi), Mustafa Mkulo (Kilosa) na Agrey Mwanri (Siha) wa CCM, Salum Barwany (Lindi Mjini) CUF na Mchungaji Israel Natse (Karatu) wa Chadema.

Kwa mujibu wa kiongozi  wa utafiti huo kutoka Repoa, Kenny Manara, amesema, utafiti huo ulifanyika mwaka 2013 na kudumu kwa mienzi mitatu hadi kukamilika.

Manara ameeleza kuwa, walianza utafiti huo baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kutoa takwimu na matumizi ya fedha kwa mwaka 2010/2011.

Anesema katika mwaka huo wa fedha, kwa mujibu wa takwimu za CAG, baadhi ya majimbo walitumia fedha zao kwa kufuatana na bajeti ilivyopagwa na mengine hayakutekeleza.

Manara amesema “katika utafiti huo, tulibaini kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa majimbo hayo hutumia fedha za wananchi kwa matumizi yao binafsi kwa kufanyinyia shughuli ambazo  hazipo kwenye bajeti kama kuchapisha vipeperushi vya kampeni na mambo mengine.

Ameongeza kuwa, waliweza kugundua chanzo cha matumizi mabaya ya mifuko ya jimbo kwamba yanasababishwa na utawala mbovu, kutofuata sheria, kutokuwepo usawa na ushirikishwaji wa wananchi.

“Viongozi wengi nchi hii wanatumia madaraka hovyo, wanatumia mifuko ya jimbo kwa manufaa yao wenyewe. Tena wengine wanajifanya wanasaidia jamii kumbe jamii yenyewe ni wafuasi wake na hii ipo katika vyama vyote vya siasa,” amesema Manara.

Kwamba, wamebaini kuwa viongozi wengi hawawashirikishi wananchi katika shughuli za kimaendeleo, kitu ambacho kinazidi kuwakandamiza watu wa chini.

“Viongozi wengi wanaomba fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika majimbo yao lakini wanatumia fedha hizo kinyume.

“Kutokamilika kwa miradi mingi nchini ni chachu ya kuongezeka kwa umaskini nchini, hivyo wananchi wanatakiwa kujipigania na kupaza sauti zao pindi wanapoona matatizo kama haya,” amesema Manara.

error: Content is protected !!