January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Azam yatupwa nje Ligi ya Mabingwa Afrika

Wachezaji wa Azam FC wakiwa nchini Sudan kabla ya mchezo wao dhidi ya Al Merreikh

Spread the love

PAMOJA na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza, timu Azam FC imeng’olewa katika michuano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa El Merreikh.

Azam FC walikuwa wakijitaji sare yoyote au wasifungwe zaidi ya bao 1-0 lakini wameshindwa kupata matokeo hayo, hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 3-2.

Katika mechi iliyochezwa leo jijini Khartoum, Sudan, Azam FC ilianza kukubali bao katika dakika ya 11 mfungaji akiwa Coffie. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza na ilikuwa ni kuhakikisha Azam wanakomaa hadi mwisho, lakini ikashindikana.

Al Merreikh ilipata mkwaju wa penalti kutokana na faulo ya Serge Wawa, lakini ikakosa, mambo yalionekana kuwa magumu kwa Azam FC katika kipindi cha pili ambayo ilitaka kujilinda zaidi.

Dofr akaifungia Merreikh bao la pili katika dakika ya 85, Mkenya Allan Wanga aliyeingia kipindi cha pili, akafunga bao la tatu katika dakika ya 90 na kuimaliza Azam.

error: Content is protected !!